Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dkt. Chyril Chami na mwenzake wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw. William Lukuvi wamemshukia Katibu
Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa na kusema kuwa anachanganya maana ya neno 'ufisadi', badala ya kulipua wenzake, anajilipua mwenyewe.
Mawaziri hao walitoa kauli hizo jana kwa nyakati tofauti walipozungumza na gazeti hili kufuatia madai ya Dkt. Slaa kwamba viongozi hao na wanasiasa wengine wanafanya ufisadi kujigawia vitalu vya kuvuna magogo katika msitu wa Sao Hill, Mafinga mkoani Iringa.
Akizungumzia madai hayo, Dkt. Chami alisema tatizo la Dkt. Slaa ni kushindwa kuelewa ukweli katika suala la vibali vya uvunaji magogo hayo na kuchanganya maana ya neno 'ufisadi'.
"Vibali vya kuvuna magogo kwenye msitu huo sio kitu cha siri, ni jambo la wazi, kila mwananchi anaruhusiwa kuomba, wanaokubaliwa majina yao yanabandikwa ubaoni ni mamia ya watu. Hapa Dkt. Slaa anakosea, anashindwa kuelewa maana ya neno ufisadi na kupotosha umma," alisema Dkt. Chami.
Alifafanua kuwa vitalu vya msitu wa Sao Hill ni mali ya serikali na havimilikiwi na mtu yeyote bali umekuwepo utaratibu wa kuvuna mbao kila mwaka ambao hauna tenda na wananchi kwa maelfu wamekuwa wakiomba na kupata vibali hivyo.
" Maelfu ya wavunaji huomba na kupata vibali vya kuvuna magogo kwa utaratibu wa kuandika barua, ni lazima uandike barua kila mwaka kuomba na kulipia kibali hicho. "
"Dkt. Slaa hawezi kuthibitisha kuwa nimejimilikisha kitalu kwasababu hakuna mtu mwenye uwezo wa kujimilikisha msitu wa serikali,"alisema Dkt. Chami na kuongeza kuwa aliomba kibali hiyo kwa nia njema ya kupata mbao za kusaidia ujenzi wa shule mbalimbali jimboni kwake.
Kwa upande wake Bw. Lukuvi alisema mbali ya mawazo yake kuwalipua mawaziri hao, Dkt. Slaa amejilipua mwenyewe kwani ameropoka jambo asilo na ushahidi wake.
Alisisitiza kuwa msitu huo ni mali ya serikali na hakuna yeyote mwenye uwezo wa kumiliki eneo ndani ya msitu huo.
"Dkt. Slaa asome hata vitabu vya sheria, msitu huu ni mali ya serikali, hakuna aliyemilikishwa. Uvunaji wake umewekwa kwenye utaratibu wa wazi kwa kila mtu, hapa ufisadi haupo!" alisema Bw. Lukuvi.
Akaongeza "Niliomba kibali ili nipate mbao za kwenda kuezeka shule ya Idodi iliyoungua kwenye jimbo langu, nilifanya hivyo kupunguza gharama za bidhaa hiyo, nikapata kibali nikavuna mbao za kutosha kama 1,000 nilipomaliza kazi hiyo sikuomba tena kibali kiliisha siku ilele. Anachozungumza Dkt. Slaa ni mambo ya mwaka juzi na hayana ufisadi wowote.
" Fedha nilizolipa kwa Idara ya Misitu kama ushuru na kodi ya kupasua mbao hizo ni 2, 835,330/- Mimi natoa ushauri wa bure kwa Dkt. Slaa asiwe mzee wa mipasho na milipuko. Katika hili, amejilipua mwenyewe baada ya kukubali kupokea maneno na kuropoka bila utafiti, aige mfano wa mbayuwayu" alisema Bw. Lukuvi na kuleza kwamba anamfahamu na kumheshimu Dkt. Slaa kutokana na huduma mbalimbali za shirika la CCBRT mkoani Iringa lakini kwa hili ameteleza.

Subscribe to: Post Comments (Atom)
15 Maoni:
Post a Comment
Links to this post