Tuesday, 23 August 2011 20:12 |
WAFANYABIASHARA wa nguo na viatu wamelalamikiwa kwa kupandisha bei ya bidhaa, wakati wa kuelekea kwenye Sikukuu ya Iddi.Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam walisema bei ya nguo na viatu vya watoto imepanda, hali itakayosababisha wazazi wengi kushindwa kumudu. “Hali imekuwa ngumu wakati huu, nguo zimepanda bei na hatuna uwezo, sijui watoto wetu watavaa nini sikukuu,” alilalamika mwanamke aliyetambulika kwa jina moja la Zubeda. Wazazi wengi wakiwa na watoto walionekana kwenye maduka, wakifanya ununuzi wa nguo na viatu. “Hawa wafanyabiashara wanafanya sikukuu ndiyo kipindi cha kuongeza mtaji na kupata faida kubwa, kitu ambacho siyo sahihi na kinatukandamiza wanyonge,” alisema Jamal Habibu Baadhi ya wafanyabiashara walisema chanzo cha kupanda bei |
Wednesday, August 24, 2011
wafanyabiashara walalamikiwa bei ya mafuta kupanda
venance.chadema@yahoo.com
Welbeck ang'ara United .
venance.chadema@yahoo.com
Tuesday, 23 August 2011 20:54 |
MSHAMBULIAJI Danny Welbeck alifunga bao moja na kutengeneza pasi ya bao lingine wakati Manchester United ilipoichapa mabao 3-0 Tottenham Hotspur katika mechi ya Ligi Kuu England iliyofanyika juzi kwenye uwanja wa Old Trafford. Katika mechi hiyo kocha wa Manchester United, Alex Ferguson aliamua kupanga wachezaji vijana ambapo vijana hao hawakumuangusha kwani Welbeck alifunga bao la kwanza baada ya kuunganisha vizuri kwa kichwa krosi ya kijana mwenzake Tom Cleverley. Katika dakika ya 76, Welbeck alitoa pasi nzuri ya kisigino akiwa ndani ya |
Mputu arudi kwa kishindo, Angola yapata kinara mpya .
venance.chadema@yahoo.com
Tuesday, 23 August 2011 20:55 |
MSIMU mpya wa ligi ya Morocco umeanza kwa mabingwa watetezi Raja Casablanca kupoteza mchezo wao wa kwanza. Recreativo Libolo ilikalia kiti cha uongozi wa ligi ya Angola huku Red Arrows ikiendeleza rekodi yao ya kutofungwa Zambia. Nchini DR Congo, TP Mazembe Englebert imeendelea kupanda kileleni. DR Congo Super League: Timu tatu kileleni Kurejea kwa Tresor Mputu baada ya kifungo cha mwaka moja aliamsha hali mpya kwenye soka la Congo, mshambuliaji huyo alionyesha umuhimu wake kwenye kikosi cha Mazembe alipoiongoza kushinda 3-0 dhidi CS Don Bosco 3-0 jijini Lubumbashi. Matokeo hayo yameifanya Mazembe kufikisha pointi 19, moja nyuma ya vinara V Club Mechi kubwa: Mputu alitangaza kumaliza kifungo chake kwa |
Sua wavumbua chanjo mpya ya wanyama .
venance.chadema@yahoo.com
Tuesday, 23 August 2011 20:24 |
CHUO Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (Sua), kimevumbua chanjo inayotibu magonjwa mbalimbali kwa kuku na wanyama wengine iliyotokana na mimea nchini. Mratibu wa Haki Miliki wa Sua, Profesa Amini Kweka, alisema chanjo hiyo imevumbuliwa na wataalamu wa chuo hicho na kutengenezwa chuoni hapo. Profesa Kweka alisema tayari wameifanyia majaribio nchi nzima na imeonyesha mafanikio makubwa kuliko dawa zingine zilizoko madukani. “Chanjo hii inatibu magonjwa mengi ya kuku na wanyama wengine, baada ya |
Yanga kwa Moro, Simba, Coastal hapatoshi
Tuesday, 23 August 2011 21:09 |
BAADA ya kushuhudia moto mkali ukiwaka kwenye ufunguzi wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara kitimtim hicho kinaendelea tena leo kwa timu 12 kushuka dimbani kumenyana kwenye viwanja sita tofauti. Kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga ikitoka kwenye majeraha ya kuchapwa bao 1-0 na JKT Ruvu kwenye mechi ya ufunguzi watakuwa na kazi ya kurudisha matumaini ya mashabiki wao wakati watakapoivaa Moro United. Katika mchezo huo, Yanga ambayo imepoteza imani ya mashabiki wake baada ya kupoteza mechi tano mfululizo tangu Julai 21 inatarajia kukutana na upinzani mkali kutoka kwa Moro United ambayo ilionyesha upinzani mkali kwenye mechi dhidi ya Azam FC licha ya kulazwa bao 1-0. Kwa upande mwingine wapinzani wa Yanga, Simba SC wenyewe watakuwa |
Gaddafi, waasi ngoma nzito
venance.chadema@yahoo.com
Tuesday, 23 August 2011 20:39 |
Juzi usiku, waasi hao walitangaza kuingia Tripoli ambako ni ngome muhimu ya Gaddafi na vikosi vyake lakini hadi jana, licha ya kiongozi huyo kutojulikana aliko huku watoto wake wa tatu waliodaiwa kukamatwa na waasi hao wakionekana mitaani, hakuna upande uliokuwa umetangaza udhibiti wa moja kwa moja wa mji huo. Katika siku hiyo ya pili ya mapambano, majeshi ya Gaddafi yamedaiwa kutumia silaha nzito wakati waasi nao wakijitangazia kusonga mbele ili kuishikilia Tripoli nzima baada ya |
ikulu yamsafisha Jairo
venance.chadema@yahoo.com
Tuesday, 23 August 2011 20:43 |
IKULU imemrejesha kazini Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo baada ya uchunguzi wa tuhuma dhidi yake za kutenga mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kuhonga wabunge ili wapitishe bajeti ya wizara hiyo, kubainika kuwa si za kweli.Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo alitangaza uamuzi huo katika mkutano wake na waandishi uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam jana akisema Jairo hana hatia na leo anapaswa kurejea kazini mara moja. Alisema matokeo ya uchunguzi dhidi yake yamebainisha kwamba hakuwa na hatia hivyo kusema kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Sheria namba 8 ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003, anamrejesha kazini Jairo... “Ninaamuru David Jairo arejee kazini kuanzia siku ya Jumatano (leo).” Julai 18, Jairo alituhumiwa na baadhi ya wabunge wakati wakichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwamba amezitaka taasisi, vitengo na idara zilizo chini ya wizara hiyo, zichangie Sh50 milioni kila moja, ili kufanikisha bajeti hiyo. Tuhuma hizo zilitolewa na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo na |
Subscribe to:
Posts (Atom)