Monday, May 30, 2011

Bin Hammam na Warner kiti moto Fifa

Fifa imeanza uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazozingira maafisa wake, akiwemo makamu wa rais Jack Warner na mgombea wa kiti cha urais wa Fifa Mohamed bin Hammam.
Mohamed Bin Hammam
Mohamed Bin Hammam
Tuhuma hizo zilitolewa na mjumbe wa kamati kuu Chuck Blazer.
Blazer amedai taratibu za maadili ya Fifa zilikiukwa katika mkutano unaoonekana uliandaliwa na Bin Hammam na Warner.
Maafisa wengine wawili ni Debbie Minguell na Jason Sylvester kutoka Muungano wa

Blatter kujitetea mbele ya FIFA


Sepp Blatter
Kujitetea Jumapili juu ya madai ya ufisadi mbele ya kamati ya maadili ya FIFA
Rais wa shirikisho la kimataifa la soka, FIFA, Sepp Blatter, itabidi kujitokeza mbele ya kamati ya shirikisho hilo inayohusika na maadili, ikiwa ni hatua ya uchunguzi wa madai kwamba maafisa wa juu wa shirikisho hilo kupokea hongo.
Blatter ameitwa na kamati hiyo pamoja na maafisa wenzake wa bodi, Jack Warner na Mohammed Bin Hammam.
Kamati hiyo itawasikiliza keshokutwa Jumapili.
Blatter ameamriwa kufika mbele ya kamati hiyo, baada ya

Bin Hammam kutowania madaraka FIFA

Mohamed Bin Hammam kutoka Qatar, ameelezea kwamba amejiondoa katika uchaguzi wa kuwania madaraka ya rais wa shirikisho la kimataifa la soka, FIFA.
Mohamed Bin Hammam
Mohamed Bin Hammam
Bin Hammam, mwenye umri wa miaka 62, alitangaza hatua hiyo saa chache kabla ya kufika mbele ya tume ya maadili kujibu madai ya kuhusika katika kupokea mlungula.
Mkuu huyo wa mashirikisho ya soka ya bara Asia, alisema nia yake ni kuliepusha jina la shirikisho la FIFA kuharibiwa sifa kwa kupakwa matope.
Bin Hammam alikuwa anatazamiwa kupambana na rais wa shirikisho hilo, Sepp Blatter, ambaye pia anachungwa na kamati hiyo ya maadili.
Wote wawili wanakanusha lawama za kupokea hongo

Barcelona klabu bingwa Ulaya

Matumaini ya mashabiki wa Manchester United pamoja na wakuu wa chama cha mpira England yalikuwa makubwa kwa Sir Alex Ferguson kutwaa kombe la pili katika msimu mmoja baada ya kushinda Ligi ya England na licha ya kushindwa kutwaa kombe la FA na la Carling.
Barcelona na kikombe baada ya mechi Wembley
Barcelona na kikombe baada ya mechi Wembley
Wayne RooneyDhamira tangu mwanzo ilikuwa ya angalau makombe matatu likiwemo Kombe la Ligi ya mabingwa wa Ulaya.
Ferguson akiwa na Kocha wa Barcelona, Guardiola
Messi katikati Fainali ya mwaka huu ikichezwa kwenye uwanja wa Wembley ilionekana kuwapendelea Manchester United ambao katika michuano yote ya kufuzu kufikia hapa hawakupoteza mechi hata moja.
Mchuano ulianza kwa vijana wa Man.united kuonyesha uwezo wa kuikaba Barcelona koo.
Hali hiyo iliendelea kwa dakika kumi za kipindi cha kwanza na mnamo dakika ya 27 Pedrito akapenya lango la Man.United
Licha ya Barca kutangulia kwa bao la Pedrito Man.united wakatumia makosa ya Barca kusinzia na Wayne Rooney kupachika bao ambalo baadhi ya wadadisi walidhani lilitokana na kosa baada ya mchezaji wa Barca kusukumwa na mpira wa Rooney kumpata Ryan Giggs katika hali ya

Mlipuko wa bomu waua 10 Nigeria

Goodluck Jonathan


Nigeria
Nigeria

Karibu watu 10 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa baada ya bomu kulipuka karibu na kambi ya jeshi Kaskazini mwa Nigeria,maafisa katika eneo hilo wamesema.
Mlipuko huo ulitokea katika soko la Mamy mjini Bauchi siku ya Jumapili.
Watu waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.
Kufikia sasa hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika na shambulio hilo.
Shambulio limetokea saa chache baada ya Goodluck Jonathan kuapishwa kwa muhula mpya wa miaka minne kama rais katika mji mkuu wa

Ujerumani kuvimaliza vinu vya nuklia

Kufuatia mazungumzo ya usiku kutwa ya serikali ya mseto nchini Ujerumani, nchi hiyo imetangaza kubadilisha sera kuhusiana na nguvu za nuklia.
Mjerumani katika maandamano
Mtu aliyebeba bango ambalo linauliza; 'Nguvu za nuklia? - La, hasha!'
Ujerumani imetangaza kwamba itakomesha utumizi wa vinu 17 vya nguvu za nuklia kufikia mwaka 2022.
Uamuzi huo unaifanya Ujerumani kuwa taifa la kwanza kubwa ambalo limeendelea sana kiviwanda kutangaza kutupilia mbali utumizi wa nguvu za nuklia.
Mataifa kadhaa yamekuwa yakizichunguza sera zake kuhusiana na nguvu za nuklia, hasa kufuatia janga la Fukushima nchini Japan, mwezi Machi.
Nchi ya Uswisi wiki iliyopita ilikuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kutangaza kwamba itasimamisha utumizi wa

Zuma kujaribu kutatua mzozo wa Libya


Jacob Zuma
Jacob Zuma
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewasili mjini Tripoli kwa kile kinachoonekana kuwa juhudi za mwisho za kujaribu kutafuta suluhu ya kidiplomasia ya mzozo unaoendelea.
Haifahamiki kama ziara hiyo ambayo ni ya pili kwa Bw Zuma, itaangazia kumshawishi Kanali Muammar Gaddafi kuondoka madarakani.
Waasi wanaopigana na majeshi ya Gaddafi tangu mwezi Februari wamekataa kufanya mazungumzo hadi pale atakapoondoka kwenye uongozi.
Wakati huo huo chama cha Bwana Zuma cha