Sunday, June 5, 2011

WILL SMITH: KAFARIKI DUNIA?

story zilizotanda kila kona ya kuwa Will Smith msanii, muigizaji na mchekeshaji amefariki kwa kuji overdoze, zimekanushwa na website mbali mbali na kudai kuwa ni uzushi tu, na si mara ya kwanza kuzushiwa kwa Will Smith ambapo mwaka jana alizushiwa kuwa amefariki kwa ajali ya gari. will smith yupo kitaa bado anaendelea kupeta kitaa na kukisanua kama kawa

Uzushi mwingine ulikuwa ni wa mtu mzima 2pac ambae alifariki dunia mwaka 1996
kama uliingia chaka na kukubali utakua mjinga, ilifikia mpaka idadi wa watu 3,000 waliingia chaka juu ya story iliyokua ikitapakaa kila sehemu ambayo ilikua ikisema tupac yuko hai na anaishi New Zealand.

Ujerumani yagundua chanzo cha E.coli.


Maharagwe yanayochipuza
Maharagwe yanayochipuza
Maafisa wa Ujerumani wanasema kuwa wanaamini maharagwe yanayokuzwa nchini humo huenda yakawa ndio chanzo cha maambukizi ya bakteria hatari ya E.coli.
Tangu mlipuko huo kuzuka, bakteria hiyo imewauwa watu 22 na kupelekea takriban watu wengine 2000 kulazwa hosipitalini.
Wataalam kuhusu maambukizi ya maradhi wamegundua kuwa bakteria hiyo ya E.coli ilitokea katika shamba moja la mimea inayoota kusini mwa mji wa Hamburg.
Waziri mmoja ameliambia shirika la habari la AP kuwa bakteria hiyo imetokana na maharagwe

Mbowe kufikishwa mahakamani Arusha, mnyika ateta, asema ni udalilishwaji, mwenyekiti wa cuf prof.Lipumba naye ang'aka, adai ni njama za kuidhoofisha kambi ya upinzani bungeni...


Dkt Freeman Mbowe
Kiongozi wa upinzani TZ, dkt Freeman Mbowe
Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Tanzania, Dkt. Freeman Mbowe, anatarajiwa kufikishwa mbele ya Mahakama moja ya Mkoa wa Arusha, Kaskazini mwa nchi hiyo.
Bw. Mbowe alikamatwa na polisi hapo jana kwa madai ya kukiuka sheria za dhamana.
Kukamatwa kwa Bw. Mbowe kunakuja siku chache baada ya mahakama moja mjini Arusha kuamuru akamatwe baada ya kukiuka dhamana.
Anashutumiwa kwa kutojitokeza kortini wakati wa kesi inayomkabili pamoja na viongozi wenzake wa Chama Cha Demokrasia (CHADEMA), ya madai ya kuandaa mkutano na kuandamana kinyume cha sheria, Januari 2011.
Hata hivyo kukamatwa kwa Dkt Mbowe kumevutia hisia kali. Mbunge wa CHADEMA John Munyika, ametaja kukamatwa kwake kama udhalalishaji. ''Ni shambulio dhidi ya

Ivory Coast yaichapa Benin 6-2, taifa stars yatandikwa 2-1 na jamhuri ya kati,.... pata matokeo mengine kwa mechi zote zilizochezwa hiyo jana pamoja na vinara wa makundi.

kombe la mataifa ya Afrika
Michuano ya soka ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika yamefanyika. Katika joto hilo Kocha wa Algeria - Abdelhak Benchikha amejiuzulu mapema leo baada ya kuchukizwa na kipigo Timu yake ilichopewa na watani wake Morocco 4-0.

Mabao ya Morocco yalipatikana kupitia Mehdi Benatia na mshambuliaji wa Arsenal Marouane Chamakh katika kipindi cha kwanza na katika kipindi cha pili mji wa Marrakech ulilipuka kwa vifijo kufuatia mabao ya Youssouf Hadji na Oussama Assaidi yaliyopatikana dakika tisa baada ya kipenga cha kuanza kipindi cha pili.
Hivyo Morocco ikalipiza kisasi cha bao moja ililofungwa katika duru ya kwanza miezi mitatu iliyopita. Morocco ina pointi saba huku Jamhuri ya kati, Tanzania na Algeria zote zina pointi nne kila moja.
kufuzu mwaka 2012
Wawakilishi wengine wa Afrika kwenye kombe la Dunia mwaka jana Cameroon walijikuta nyuma ya Senegal kwa pointi tano baada ya kutoka sare ya 0-0 nyumbani mjini Yaounde hapo jana.
Ilibidi Polisi watumie gesi ya

3 Juni 2011 Amri ya Kumkamata Kiongozi wa kambi Rasmi ya Upinzani yaingilia uhuru wa Bunge, yahatarisha demokrasia!!


Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imepokea kwa mshtuko, masikitiko na mshangao mkubwa taarifa za Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha kutoa amri ya kumkamata Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe. Mheshimiwa Mbowe pamoja na Wabunge, viongozi na wanachama kadhaa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanakabiliwa na mashtaka kadhaa yanayotokana na maandamano tarehe 5 Januari 2011 katika Jiji la Arusha yaliyopelekea Jeshi la Polisi kuua wananchi watatu na kujeruhi wengine wengi. Taarifa zinaonyesha kwamba amri hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Charles Magessa, siku ya Ijumaa ya tarehe 27 Mei 2011 na kurudiwa tena jana, yaani tarehe 2 Juni 2011.
Mheshimiwa Mbowe hakuhudhuria mahakamani katika tarehe zote mbili kwa vile amekuwa akihudhuria vikao vya Kamati mbali mbali za Bunge vilivyoanza tarehe 23 Mei 2011 na ambavyo vinaendelea hadi hivi sasa kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaotazamiwa kuanza tarehe 7 Juni hadi tarehe 7 Septemba 2011. Kama Mbunge na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Mbowe ni mjumbe wa Kamati mbali mbali za Bunge kama vile Kamati ya Uongozi, Kamati ya Kanuni za Bunge na Kamati ya Fedha na Uchumi. Aidha, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ni mjumbe katika Tume ya Utumishi wa Bunge na ndiye msemaji mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na amri ya kumkamata Mheshimiwa Mbowe kwa vile inakiuka moja kwa moja sheria, mila na desturi za miaka mingi zinazohusu kinga, haki na mamlaka ya Bunge na

MKUTANO WA CHADEMA KIGAMBONI WAAHIRISHWA KUTOKANA NA KUKAMATWA KWA MWENYEKITI WA CHAMA HICHO MH. FREEMAN AIKAELI MBOWE NA NAIBU KATIBU MKUU MH. ZITO ZUBERI KABWE.

Mkutano wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, uliokuwa ufanyike katika kata ya Kigamboni wilayani temeke umeahirishwa kutokana na waheshimiwa wabunge wa chadema waliotarajiwa kuwepo katika mkutano huo kutokufika.
 MH. Rozi Wilbard, mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke baada ya kuahirishwa kwa mkutano huo.
 Mwanaharakati anayechipukia VENANACE MREMA(supersonic) akiwa na mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Temeke mh. ROZI WILBARD baada ya mkutano huo kuahirishwa.
 Mmoja wa makada wa chama aliyehudhuria mkutano huo, akishushwa jukwaani mara baada ya kupatwa  na mshtuko wakati wa maandalizi ya mkutano huo hapo leo.
 Askari wa kituo cha polisi cha KIGAMBONI akiwasili uwanjani hapo mara tu baada ya mkutano huo kuahirishwa, kama kawaida kila inapokuwepo mkutano wa CHADEMA mambo kama hayo huwa hayakosekani.
 Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Temeke bi Rozi Wilbard akilizungumzia kwa machungu swala la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa chama cha Chadema MH. FREEMAN MBOWE.
 Mwanaharakati anayekuja juu kwa kasi VENANCE MREMA(supersonic), akiwa na mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Temeke Bi.ROZI WILBARD mara baada ya kuahirishwa kwa mkutano huo.
 wanaharakati mashuhuri nao hawakuwa nyuma katika kuzielezea hisia zao katika mkutano huo.
 Baadhi ya wakereketwa wa demokrasia waliohudhuria katika mkutano huo.
 Mmoja wa makada wa CHADEMA aliyepata stress kabla ya kuanza kwa mkutano huo hapo leo.
Akizungumza na wananchi waliofika katika viwanja hivyo mwenyekiti wa chama hicho katika wilaya ya temeke mh.  Rozi Wilbard amesema waheshimiwa wabunge hao akiwemo mh.Wenje na Joseph Mbilinyi walishindwa kuwepo kutokana na kuwepo katika kikao na kamati kuu ya chama ili kujadiliana juu ya kukamatwa mwenyekitiwa chama hicho mheshimiwa Freeman Mbowe. mh. Mbowe alikamatwa jana jioni baada ya amri kutoka kwa mahakama kwa madai kuwa alifanya mikutano ya hadhara bila kibali kinyume cha sheria na pia kudaiwa kuchochea maandamano.Aidha bi Rozi hakutanabaisha ni linimkutano huo utatangazwa tena.

Wilshere hafai kucheza Denmark


Jack Wilshere
Hatakuwepo katika michuano ya Ulaya kwa vijana chini ya umri wa miaka 21
John Terry ameunga mkono hatua ya kutomshirikisha Jack Wilshere katika kikosi cha England cha vijana chini ya umri wa miaka 21, na ambacho kitapambana katika michuano ya Ulaya baadaye mwezi huu, ikiwa ni hatua ya kumzuia kuchoka mno kupita kiasi.
Terry, nahodha wa timu ya England, alisema kiungo huyo wa kati wa klabu ya Arsenal ni "sehemu kubwa" ya timu ya taifa, na watamhitaji sana iwapo England itafuzu kwa

Gaidi maarufu auwawa Pakistan

Taarifa kutoka Waziristan Kusini zinaonesha kuwa mpiganaji wa daraja ya juu wa Pakistan, Ilyas Kashmiri, aliuliwa jana usiku katika shambulio la ndege ya Marekani, isiyokuwa na rubani.
Ndege ya Marekani isyokuwa na rubani, drone
Ilyas Kashmiri alikuwa kiongozi wa Harkatul Jihan al-Islami, kikundi cha msimamo mkali kinachoshirikiana sana na al-Qaeda.
Ametuhumiwa kuhusika na mashambulio mengi pamoja na shambulio maarufu la karibuni, dhidi ya kituo cha jeshi la wanamaji la Pakistan, mjini

Libya inashambulia helikopta za NATO

Helikopta za Uingereza zilizotumika kwa mara ya kwanza kurusha makombora dhidi ya sehemu za Libya zimeshambuliwa na jeshi la Kanali Gaddafi.
Mashua wanawaondoa wakimbizi kutoka lIbya
Mwandishi wa BBC kwenye manuwari ya jeshi la wanamaji la Uingereza, Royal Navy, katika pwani ya Libya, anasema helikopta mbili za aina ya Apache katika manuwari hiyo, zilishambulia kituo cha radar na kituo cha ukaguzi cha

Wareno wapiga kura katika uchaguz

Wagombea Coelho na Socrates
Wagombea Coelho na Socrates
Watu wa Ureno wanapiga kura katika uchaguzi ulioitshwa mapema, baada ya serikali ya kisoshalisti, kuomba mikopo kutoka vyombo vya fedha vya kimataifa, kusaidia uchumi wa nchi hiyo.
Kampeni ya uchaguzi imegubikwa na sera za kukata matumizi na

Rais Saleh huenda atarudi Yemen

Afisa mmoja mwandamizi alisema atarudi nyumbani baada ya siku chache, lakini upinzani umeahidi kuwa watamzuwia, na kuna tetesi nyingi kuwa utawala wake wa miaka 30, pengine ndio umekwisha.
Rais Ali Abdullah Saleh
Waandamanaji wakisheherekea kuondoka kwa Rais Saleh
Waandamanaji wakisheherekea kuondoka kwa Rais Saleh
Maelfu ya Wayemen wanasherehekea kuondoka kwa Rais Saleh nchini.
Vijana wengi walisherehekea katika Medani ya Chuo Kikuu cha Sanaa, na

UKIMWI uligunduliwa mwaka 1981

HIV
HIV
Mwaka wa 1981, daktari mmoja wa California Marekani aliona vijana wa kiume watano, walioshiriki katika mapenzi ya jinsia moja, wakiwa na ugonjwa usiokuwa wa kawaida.
Walikuwa na homa ya pneumonia na saratani ya ngozi.
Dakta Gottlieb hakujua kuwa ripoti zake, ndio zitakuwa historia ya

Mbowe akamatwa mjini Dar es Salaam.

Freeman Mbowe
Freeman Mbowe
Nchini Tanzania kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Chadema, amekamatwa mjini Dar es Salaam.
Freeman Mbowe anakabili mashtaka ya kufanya mkutano bila ya