Wednesday, August 17, 2011

Kago ruksa leo

venance.chadema@yahoo.com

 
Tuesday, 16 August 2011 20:16


SHIRIKISHO la Soka Tanzania ( TFF) limesema kuwa linasubiri majibu kutoka kwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuhusu klabu ya Simba kumtumia mchezaji wao mpya, Gervais Kago kama ataweza kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

Kago aliyesajiliwa akitokea klabu ya Olympic Real de Bangui ya Jamhuri ya

Vita ya Barcelona, Madrid yahamia Camp Nou .

venance.chadema@yahoo.com

 Send to a friend
Tuesday, 16 August 2011 20:11
BARCELONA, Hispania
LEO ni fainali ya Hispania Super Cup, ambapo Barcelona itakuwa ikikabiliana na Real Madrid katika mechi ya pili ya kuwania kombe hilo baada ya timi hizi kukutana kwa mara ya kwanza Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu na kutoka sare ya 2-2.

Katika mechi ya kwanza iliyozikutanisha Real Madrid na Barcelona ya kuwania Hispania Super Cup siku ya Jumapili, timu ya Real Madrid ilipiga mashuti mengi golini, lakini mabingwa wa Ulaya na mabingwa wa Ligi Kuu ya Hispania wao walipata faida ya magoli mawili ya ugenini

Mechi ya Simba vs Yanga:Majigambo yatawala Facebook

venance.chadema@yahoo.com


Tuesday, 16 August 2011 20:15

Vicky Kimaro
MAJIGAMBO ya mechi ya Ngao ya Jamii baina ya Yanga na Simba jana yalitawala katika mtandao wa kijamii wa facebook ambako wachezaji na mashabiki walikuwa wakitupiana vijembe.

Kupitia mtandao huo ambao unasomwa na maelfu ya watu duniani kote, mchezaji wa Yanga, Rashid Gumbo alianza kwa kuandika ujumbe mfupi wa kujinadi kuwa watashinda mchezo huo huku akiwapiga kijembe watani zao Simba kuwa wanapenda kulaumu kufuatia kitendo cha mchezaji wao

SIMBA VS YANGA:Hapa vumbi tu

venance.chadema@yahoo.com


Tuesday, 16 August 2011 20:22

Sosthenes Nyoni
MAHASIMU wa kihistoria katika soka la Tanzania, timu za Simba na Yanga leo zitaingia katika vita nyingine pale zitakaposhuka dimbani kukabiliana  katika mechi ya kuwania Ngao ya Jamii itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mpambano huo unaoashiria ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu itakayoanza Jumamosi hii, unatarajiwa kuwa na upinzani mkali huku ukiwa unafanyika takribani siku 36 tu tangu timu hizo zilipokutana katika mechi ya fainali ya michuano ya

Chadema waivaa rasmi CCM uchaguzi Igunga

venance.chadema@yahoo.com


Tuesday, 16 August 2011 21:09


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza rasmi mapambano na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga baada ya kumwandikia barua msimamizi wa uchaguzi huo kikimtuhumu Mweka Hazina wa chama hicho tawala ngazi ya taifa, Mwigulu Nchemba kuanza kumwaga misaada yenye lengo la kile ilichodai ni kushawishi wapigakura.

Hatua hiyo ya Chadema kuandika barua rasmi kuelezea tuhuma hizo, imekuja wakati tayari vyama hivyo viwili vikiwa katika malumbano ya maneno kila kimoja kikikishutumu kingine kucheza mchezo mchafu kabla ya muda wa kampeni uliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).

Chadema kiliandika barua hiyo yenye kumbukumbu namba  CDM/W/IG/UCH/Vol.1/201 Agosti 15, mwaka huu na kusainiwa na katibu wa chama hicho

Tibaijuka awatisha Malecela, Sumaye, AONYA MUDA WAO KUHODHI ARDHI KUBWA UMEKWISHA

venance.chadema@yahoo.com

Tuesday, 16 August 2011 23:34


Waandishi wetu, Dodoma, Dar
LICHA ya kupata wakati mgumu Bungeni, Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imepitishwa jana huku Waziri wake, Profesa Anna Tibaijuka akitoa onyo kwa wanaohodhi ardhi kwa muda mrefu bila kuiendeleza akisema: “Fungate yao imekwisha.”

Kauli hiyo ya Profesa Tibaijuka imekuja siku moja baada ya kambi ya upinzani bungeni kupitia Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee kutaja orodha ndefu ya vigogo hao wa CCM wakiwamo Marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Mawaziri Wakuu wastaafu, John Malecela na Frederick Sumaye.

Wengine waliotajwa ni Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Philip Mangula na aliyekuwa Naibu wake (Bara), Hassan Ngwilizi akisema kwamba wamehodhi ardhi kubwa mkoani Morogoro bila kuiendeleza. Hata hivyo, alisema ni