venance.chadema@yahoo.com
Tuesday, 16 August 2011 20:15 |
Vicky Kimaro
MAJIGAMBO ya mechi ya Ngao ya Jamii baina ya Yanga na Simba jana yalitawala katika mtandao wa kijamii wa facebook ambako wachezaji na mashabiki walikuwa wakitupiana vijembe.
Kupitia mtandao huo ambao unasomwa na maelfu ya watu duniani kote, mchezaji wa Yanga, Rashid Gumbo alianza kwa kuandika ujumbe mfupi wa kujinadi kuwa watashinda mchezo huo huku akiwapiga kijembe watani zao Simba kuwa wanapenda kulaumu kufuatia kitendo cha mchezaji wao Gervais Kago kuzuiwa kucheza mchezo huo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa madai kuwa hawakufuata kanuni za usajili.
Ujumbe wa Gumbo ulikuwa: "mnachojua lawama tu na sio utendaji wa kazi nyieeee..........!!!!!!! ujumbe huo uliungwa mkono na mchezaji wa Azam Fc Himid Mao.
Lugano James: umewaona eeeeeeeeeeeeeeeee
Hussein Jamaldin: Wapi nyie ndo mnavyojidanganya kwa taarifa yenu tunaingia uwanjani kuwakata midomo sisi ndio watoto wa mjini kaka...!!!
Jerry Santo: "Ya mkosaji mkosaji kazi mtaiona kesho.
Jerry Santo: Zamu ya mnyama j.5 yebo yebo hamna timu pale mchezaji Berko peke yake, lakini lazima tumpeleke nyavuni kama mara tatu hivi.
Frank Maxmilian: Acha waseme tu kaka, lakini najuwa watanyamaza tu hiyo kesho watabana na kuachia kama kawaida yao
Rashid Gumbo: Mmh mnyama asie na meno nyie kama pilipili hoho hata uweke 100 kamwe aziwashi.
Manchu Movich: Hapooooooo.....Kesho Mafisango anapokamata viungo wote wa Yanga na kumpa mpira Okwi anapiga krosi kumkuta Sunzu goooooooal!!!
Himid Mao: kweli fundi hasa bongo.
Kabali Faraji: Pamoja na mipango mnayoandaliwa na TFF kuidhoofisha Simba kipigo kama kawa hakuna sababu ya msingi ya kumzuia Kago asicheze mechi hiyo ni fitna tu.
Fadhila Lemba: sijauona uzuri wa Kago wa kuifanya beki yaYanga ishindwe kucheza,Yanga hakuna majungu hakuna kulaumu mnalaumu sana ila wakilaumu wenzenu mnaona hawana akili sasa leo kwenu kazi kwenu, hamna lolote njooni uwanjani mpukutishwe manyoya.
Fadhila Lemba: tatizo mwezi mtukufu hamuendi kuroga sasa mnatumia suala la Kago kama kisingizio amkeni mpira siyo ushirikina nyie, Man City waliingia bila Aguero iweje nyie muogope?
Jerson Tegete: anko lawama kaumbiwa binadamu hujawazoea tu
Haji Hassani: Lawama sio mzigo mkali wangu
Jerry Santo: Ukipigwa kesho naomba uendelee kupost hivyo hivyo. Wewe unalaumiwa na nani au unaongea kwa niaba ya nani?.
Andry Iniesta: kwanini tuandikie mate wakati wino upo brother tumebakiza saa kadhaa tu mpigike.
Clarence Masaki: Wataisoma kesho,Gumbo ukisaidiana na Fabrigas embu watupieni mipira wakina Tegete, Asamoah na Kiiza pale mbele then tuwaduwaze vitatu hawa jamaa. |
No comments:
Post a Comment