Send to a friend |
Wednesday, 22 June 2011 21:34 |
Festo Polea MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika shule moja ya msingi ya jijini Dar es Salaam, inayotoa elimu yake kwa lugha ya Kiingereza, amejeruhiwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kuchapwa bakora akiwa uchi. Habari zilidai kuwa kitendo hicho dhidi ya mwanafunzi wa kike, kimefanywa na mhudumu wa usafi katika mabweni ya watoto.Inasemekana kuwa mtoto huyo alichapwa Juni 14 mwaka huu, baada ya kukataa kufua nguo yake ya ndani, aliyoikuta ikiwa imetapakaa kinyesi cha mtu ambaye hakufahamika. Kubainika kwa ukatili dhidi ya mtoto huyo, kumekuja baada ya mama yake mzazi, Teddy Salimwe, kuamua kumtembelea Juni 20 mwaka huu kwa lengo la kumjulia hali.Akizungumza na mwandishi wa habari hii jana, Teddy alisema alipokutana na mtoto wake, aliamua kumpakata lakini mtoto alikuwa |