Send to a friend |
Thursday, 09 June 2011 23:37 |
Neville Meena, Dodoma KAMBI ya Upinzani Bungeni imedai kwamba kuna upotoshaji mkubwa katika Bajeti ya Serikali iliyowasilishwa bungeni juzi na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, huku ikidai kwamba bajeti hiyo ni ya kulipa posho na madeni. Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Kambi hiyo mjini Dodoma na kusainiwa na Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe inabainisha kuwa upembuzi uliofanywa umebaini kuwapo kwa upotoshaji mkubwa wa kitakwimu na kimaudhui uliofanywa kwalengo la kuwajengea matumaini wananchi. "Kambi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na kushangazwa na hatua ya Serikali kutenga zaidi ya robo ya bajeti kulipa madeni na kulipana posho (asilimia 27), asilimia 14 kulipa madeni na asilimia 13 kulipa posho mbalimbali," ilisema taarifa hiyo. Miongoni mwa maeneo ambayo yanadaiwa kuwa na upotoshaji ni kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la umeme, ongezeko la jumla la Bajeti ya Serikali ikilinganishwa na ile ya mwaka 2010/11, posho mbalimbali, faini kwa madereva wazembe na ulipaji wa madeni ya Serikali. Hakuna mradi mpya wa umeme Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tamko la Serikali kwamba imetenga kiasi cha Sh537 bilioni kwa ajili ya kutatua tatizo la umeme, si kweli kwani kwa jumla Wizara ya Nishati na Madini, imetengewa Sh402.071 bilioni na kwamba hakuna mradi mpya wa umeme hata mmoja utakaoanzishwa. "Fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya matumizi ya kawaida Sh76,953,934,000 na kwa upande wa bajeti ya maendeleo zimetengwa Sh325,448,137,000. Sh325 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa 160 MW, 100 Dar es Salaam na 60 Mwanza,"inaeleza sehemu ya |