Tuesday, June 14, 2011

Mahakama yaamuru Askofu Mokiwa, Hoyay wakamatwe.


 Send to a friend
Monday, 13 June 2011 22:27
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa
Mussa Juma, Arusha
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imeagiza kukamatwa mara moja na kufikishwa mahakamani, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa na Askofu mpya wa Kanisa hilo aliyewekwa wakfu juzi, Stanley Hotay.Askofu Mokiwa, alimweka wakfu Hotay Jumapili, siku mbili tangu Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutoa maagizo ya kusitishwa kwa shughuli hiyo.

Kitendo hicho cha Askofu Mokiwa kuendelea na mchakato wa kumweka wakfu Askofu Hotay pamoja na amri ya Mahakama kutaka shughuli hiyo isitishwe, kimeelezwa kuwa ni dharau kwa mahakama.

Sherehe za kuwekwa wakfu Askofu huyo zilifanyika juzi Makao Makuu ya Dayosisi ya Mount Kilimanjaro na zilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdore Shirima, Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Claudio Bitegeko na maofisa kadhaa kutoka vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Uamuzi wa kukamatwa kwa maaskofu hao, ulitolewa jana na Jaji Kakusulo Sambo baada ya wakili wa mashtaka, Meinrad D’souza kuwasilisha maombi maalumu ya kutaka Mahakama Kuu itoe adhabu kwa Dk Mokiwa na Hotay kwa kukaidi amri ya Mahakama.

Akitoa uamuzi ambao ulichukua takriban saa moja, Jaji Sambo alisema haihitaji elimu ya chuo

TUTAMFUKUZA ZITO, SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA


 Send to a friend
Monday, 13 June 2011 22:33

Zitto Kabwe
Waandishi wetu
VITA ya kufutwa posho za wabunge na watumishi wengine wa umma, imechukua sura mpya, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kusema kwamba Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe anaweza kufukuzwa ubunge kwa kutosaini karatasi za mahudhurio.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge baada ya kuahirisha mkutano wa asubuhi, Makinda alisema Zitto anaweza kukumbwa na adhabu hiyo iwapo hatasaini karatasi za mahudhurio ambazo ndizo zinazothibitsha uwepo wa mbunge katika mikutano na vikao vyake.

"Kwa mujibu wa kanuni zetu, asipohudhuria mara tatu anakabiliwa na adhabu tena ya kufukuzwa bunge, hizo ndivyo kanuni zinavyosema." Hata hivyo, Zitto amepuuza kauli hiyo ya Spika akisema kwamba kama ni kwa ajili ya kukataa posho, yuko tayari kufukuzwa bungeni.

"Nitafanya hivyo tuone. Kanuni inasema mikutano mitatu mfululizo na siyo vikao vitatu mfululizo. Nitatumia uzoefu wangu wa siasa za wanafunzi kukwepa mtego wake. Lakini kama anadhani ni sawa kunifukuza ubunge kwa kukataa posho, nipo tayari," alisema Zitto.

Kauli ya Makinda inafuatia msimamo wa Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), kukataa