Tuesday, August 9, 2011

Fundisho: Rooney ajipanga kuitesa zaidi Man City.

Imewekwa:: 2011-08-09 09:38:00



Nyota wa Manchester United, Wayne Rooney
LONDON, ENGLAND
NYOTA wa Manchester United, Wayne Rooney amesema kikosi chake kimetoa somo kubwa kwa majirani zao baada ya kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 kwenye mechi ya kuwania Ngao ya Hisani iliyochezwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Wembley.

Manchester City walikuwa mbele kwa mabao 2-0 lakini Manchester United walikaza msuli na kufunga mabao matatu.

"Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani timu yetu ni bora,''alisema Rooney "Tulitawala mechi nzima, tumewaonyesha kwamba sisi ni zaidi. Sisi ni mabingwa na tulitaka kuthibitisha hilo

SIMBA DAY: Simba! Simba! Aaah!

venance.chadema@yahoo.com


Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange akichezea timu ya viongozi wa Simba, akimdhibiti Abdallah Ally wa timu ya makocha wa Arusha, Imam Ally wakati wa mechi ya ufunguzi wa Simba Day kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha jana Jumatatu.
MICHAEL MOMBURI,ARUSHA
SIMBA..Simba! Aaah! Ndiyo kilichotokea wakati mashabiki wa Simba wakishangilia pasi za timu yao ilipocheza na Victors ya Uganda lakini ghafla wakanywea.

Kikosi kikicheza kwa mara ya kwanza kikiwa kamili baada ya usajili kukamilika ndani ya ardhi ya Tanzania Bara, Simba ilionyesha mabadiliko lakini ikalala kwa bao 1-0 mbele ya Victors ya Uganda jana Jumatatu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Kocha Moses Basena alilaumu washambuliaji wake kwa kuwataja kwa majina Uhuru Seleman, Emanuel Okwi na Felix Sunzu kwa kukosa nafasi za wazi ambazo zingeweza kuwapa raha zaidi mashabiki katika mchezo huo ambao beki wa zamani wa Simba, Joseph Owino alikuwa jukwaani akishuhudia

Harusi ya Mercy Johnson yanukia

venance.chadema@yahoo.com


Muigizaji nguli wa Nollywood Mercy Johnson
Zimebaki wiki chache tu kufikia harusi ya Mercy Johnson lakini mambo
yamembadilikia, imedaiwa kuwa mchumba wake alimficha mambo mengi
kuhusiana na mkewe wa zamani na sasa ameyagundua.

Alichogundua ni kwamba mumewe alifunga harusi kabisa na mwanamke huyo

ingawa alimwambia Mercy kwamba ni feki zilikuwa ni picha za magazetini
tu za kutengeneza.

Lakini msanii huyo amekasirika na kutishia kwenda kanisani kufuta ndoa
hiyo kama hataweka mambo wazi na kusema kila kitu kilichojiri, lakini
inadaiwa ndugu wa mumewe wanahangaika kuweka mambo sawa.

Rooney: Tumewaonyesha City sisi ni mabosi

venance.chadema@yahoo.com


Monday, 08 August 2011 20:44

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney amesema timu yake imewaonyesha wapinzani wao Manchester City kwamba nani ni bosi nchini England baada ya juzi kuwachapa mabao 3-2 na kutwaa Ngao ya Jamii.

"Matokeo haya yanaonyesha ni timu ipi bora, katika mechi nzima tulitawala sisi na hata tofauti iliyoonyeshwa na wachezaji wetu vijana ilikuwa kubwa, tuliwasambaratisha, matokeo tuliyopata tunastahili, sisi ni mabingwa, tulitakiwa kushinda na tulitakiwa kuthibitisha hilo,"alisema

Warembo Miss Tanzania waingia kambini




Monday, 08 August 2011 20:47

WAREMBO 30 kutoka kanda tofauti nchini  jana walianza rasmi kambi ya Vodacom Miss Tanzania 2011 kwa ajili ya fainali zilizopangwa kufanyika Septemba 10 kwenye ukumbi wa Mlimani City  jijini.

Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza alisema kuwa sababu kubwa ya kuanzisha utaratibu mpya ni kuwapa nafasi zaidi warembo hao kujifunza mambo mengi wakiwa kambini kama mashindano ya “Big Brother Africa”.

Rwehumbiza alisema kuwa mfumo huu ni tofauti na  ule uliozoeleka

Viongozi CUF wanusurika ajalini

venance.chadema@yahoo.com

Monday, 08 August 2011 21:27

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro na abiria wengine watano waliokuwa wakisafiri kutoka Igunga walikofanya maandalizi ya uchaguzi mdogo kuelekea Dar es Salaam wamenusurika kifo katika ajali mbaya ya gari.

Ajali hiyo ilitokea jana jioni kilomita karibu  10 kutoka mjini Morogoro barabara ya kuelekea Dar es Salaam na kumsababishia majeraha kiongozi huyo na abiria wake.

Akizungumza na Mwananchi jana jioni katika eneo la ajali Mtatiro alisema kuwa gari waliyokuwa nayo aina
venance.chadema@yahoo.com
Mtoto aliyeibwa Bunda miaka saba iliyopita apatikana nchini Kenya
Sunday, 07 August 2011 21:50

 KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mtoto aliyeibwa wilayani Bunda, mkoani Mara miaka saba iliyopita, amepatikana nchini Kenya, baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa amemwiba kuugua na kufariki dunia.

Mtoto huyo wa kiume Nyambibiti Lazaro, ambaye sasa hajui lugha yoyote tofauti na kijaluo, aliibwa na mwanamke wakati huo akiwa na umri wa miezi minne, wakati mama yake mzazi alipokuwa amemwacha nyumbani kwao, akiwa chini ya uangalizi wa mtoto mwenzake mwenye umri wa

Madiwani waliotimuliwa Chadema wajipanga kwenda mahakamani .

venance.chadema@yahoo.com


Monday, 08 August 2011 21:28

KUNA uwezekano wa madiwani watano wa Chadema, waliovuliwa uanachama na kamati kuu ya chama hicho mwishoni mwa wiki iliyopita kwenda mahakamani kupinga uamuzi huo.

Uwezekano huo ulielezwa na Diwani wa Kata ya Elerai, John Bayo,
alipozungumza kwa njia ya simu akiwa njiani kutokea Dodoma walipokwenda kuhojiwa kabla ya uamuzi wa kutimuliwa kufikiwa.
“Binafsi sina kinyongo na chama changu wala viongozi wake. Nimepokea uamuzi huo kwani ndiyo msimamo wa vikao, lakini nakuhakikishia bado nina imani ya kuendelea na nafasi yangu ya udiwani hadi uchaguzi mkuu ujao, kuna njia nyingine ya kupinga uamuzi huo kupitia vikao au

Uchunguzi tuhuma za Jairo ngoma nzito

venance.chadema@yahoo.com


Monday, 08 August 2011 21:30
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amesema uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, unaendelea na siku kumi zilizotolewa hazitoshi.

Awali, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, akizungumzia hatua za haraka za Serikali kushughulikia kashfa hiyo, ilisema uchunguzi huo dhidi ya Jairo ungetumia siku 10, lakini Julai 31, ambayo ilikuwa ni siku ya kumi, CAG Utouh alisema ndiyo kwanza alikuwa na siku ya tano tangu kuanza ukaguzi.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Utouh alisema uchunguzi siyo kuandika ripoti, kwani

Serikali, wauza mafuta sasa wafikia pabaya .

venance.chadema@yahoo.com    Monday, 08 August 2011 21:35

  [Kituo cha kuuzia mafuta cha BP Upanga kikiwa tupu kutokana na kile kianchoelezwa kuIshiwa na mafuta, kwa zaidi ya siku nne vituo vinavyomilikiwa na BP haviuzi mafuta, bada ya mgomo uliondeshwa nchi nzima na wauza mafuta waking EWURA kupunguza bei ya bidhaa hiyo kutokana na serikali kuwapunguzia kodi ilikuleta unafuua kwa wananchi. Picha na Fidelis Felix ]  Kituo cha kuuzia mafuta cha BP Upanga kikiwa tupu kutokana na kile kianchoelezwa kuIshiwa na mafuta, kwa zaidi ya siku nne vituo

Spika amtwisha Zitto Kabwe zigo la UDA.

venance.chadema@yahoo.com

Monday, 08 August 2011 23:06

Zitto Kabwe

SAKATA la kuuzwa kwa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) limezidi kugonganisha vichwa vya mamlaka mbalimbali, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhamisha mchakato wa uchunguzi huo kutoka Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwenda Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).Utata wa uuzaji wa shirika hilo umesababisha pia mvutano mkubwa kati ya wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam na Meya wa jiji hilo, Dk Didas Masaburi ambaye wiki iliyopita aliwashambulia wawakilishi hao kwa maneno makali huku akitoa vitisho kwamba atalipua tuhuma zao za ufisadi.

Makinda aliikabidhi jukumu hilo POAC Ijumaa ya Agosti 5, Spika na kuliondoa Kamati ya Miundombinu ambako Profesa Juma Kapuya ambaye ni mmoja wa wajumbem, ana maslahi na UDA kutokana na kuwa mmoja wa wanahisa wa Kampuni ya Simon Group.
 
Kaimu Katibu wa Bunge John Joel alithibitisha jana Spika amefanya