Tuesday, August 9, 2011

Rooney: Tumewaonyesha City sisi ni mabosi

venance.chadema@yahoo.com


Monday, 08 August 2011 20:44

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney amesema timu yake imewaonyesha wapinzani wao Manchester City kwamba nani ni bosi nchini England baada ya juzi kuwachapa mabao 3-2 na kutwaa Ngao ya Jamii.

"Matokeo haya yanaonyesha ni timu ipi bora, katika mechi nzima tulitawala sisi na hata tofauti iliyoonyeshwa na wachezaji wetu vijana ilikuwa kubwa, tuliwasambaratisha, matokeo tuliyopata tunastahili, sisi ni mabingwa, tulitakiwa kushinda na tulitakiwa kuthibitisha hilo,"alisema Rooney.

Alisema,"Manchester City walitaka kuthibitisha kwamba wao ni timu ambayo inataka kutwaa ubingwa wa England msimu huu, lakini sisi tulianza kwa kutawala sana katika kipindi cha kwanza, ila katika kipindi hicho walitufunga mabao mawili ya haraka haraka hata sijui yalitoka wapi hivyo tulionyesha uwezo wetu na kushinda mechi."

Naye kocha wa Manchester United, Alex Ferguson akilizungumzia pambano hilo alisema amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake vijana ambao walibadilisha kabisa aina ya uchezaji uwanjani.

Ferguson alifanya mabadiliko na kuwaingiza Phil Jones, Jonny Evans na Tom Cleverley na baadaye alimuingiza Rafael, ambapo wastani wa wachezaji wake waliokuwapo uwanjani kuanzia dakika ya 71 ulikuwa wa umri wa miaka 22, lakini baadaye alimuingiza Berbatov.

"Kwetu sisi nafikiri mchezo huo umeonyesha jinsi tunavyofikiri, watu walikuwa wakisema kikosi cha Manchester United hivi sasa siyo kikosi bora na mengi mengine, lakini unatakiwa kukumbuka kwamba vijana huwa wanaongezeka kiwango, sisi Manchester United tunaamini tutafanya vizuri na kundi hili la vijana tulilonalo,"alisema Ferguson.Kuhusu kipa wake David de Gea ambaye alioneka kushindwa kuzuia krosi ambayo ilimkuta Joleon Lescott aliyejitwika na kufunga bao la kwanza halafu pia alishindwa kuzuia shuti la mbali la Edin Dzeko  ambalo lilikuwa bao la pili, kocha Ferguson alisema,

"City ni timu kubwa na upigaji wa mipira yao ni mzuri, kipa wetu  alikuwa hana nafasi ya kuweza kuzui mipira ile."
"Bao la pili tulilofungwa mabeki walikuwa na uwezo wa kuzuia, lakini hawakuzuia, ambapo mpira ulimkuta kipa katika nafasi ngumu ya kuweza kuzuia,"alisema Ferguson.

Kwa upande wa kocha wa Manchester City, Roberto Mancini ambaye alikuwa na wachezaji wake wakiangalia wakati Manchester United wakikabidhiwa ngao alijikuta akipata wakati mgumu kujibu maswali baada ya kumtoa Mario Balotelli katika dakika ya 58, ambapo mchezaji huyo alitoka uwanjani na kwenda moja kwa moja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na hakurudi tena kukaa kwenye benchi.

Manchini alisema,"alipoenda kwenye vyumba vya kubadilishia ngua hakuna kiongozi yoyote aliyemuambia atoke nje, kila wakati Mario akifanya kitu watu wanafuatilia, lakini Mario anaweza kucheza soka kuliko alivyocheza katika mechi hii dhidi ya Manchester United."

Akizungumzia pambano lao lilivyokuwa, Manchini alisema,"nafikiri Manchester United walicheza vizuri kuzidi sisi, kwa sababu unapokuwa unaongoza kwa mabao 2-0 unachotakiwa kufanya ni kutawala mchezo, labda matokeo mwishoni yalitakiwa kuwa 2-2 lakini soka ndivyo ilivyo,"alisema Mancini.

Alisema,"Manchester United ni timu kubwa kuliko timu nyingine England, lakini bado tuna matumaini ya kutwaa ubingwa wa England."

Wakati huo huo, kocha wa Manchester United, Alex Ferguson alisema mshambuliaji wake Danny Welbeck aliumia kifundo cha mguu katika mechi hiyo na hivyo hata kuwapo katika kikosi cha England kitakachocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Holland kesho.

No comments:

Post a Comment