Wednesday, May 25, 2011

Mjue Kizza Besigye

 Bw Besigye anamuita kiongozi huyo wa Uganda "dikteta".

Kizza
Kizza Besigye

Kizza Besigye alikuwa daktari binafsi wa Rais Yoweri Museveni. Lakini sasa Bw Besigye anamuita kiongozi huyo wa Uganda "dikteta".
Bw Besigye analalamika kuwa wafuasi wake wananyanyaswa na kuambiwa hawatapatiwa misaada na serikali, ingawa hakukamatwa wakati wa uchaguzi, na aliweza kufanya kampeni zake.
Baada ya kurejea Uganda, kabla ya uchaguzi wa mwaka 2006, alikamatwa na kushitakiwa kwa uhaini na ubakaji.
Dokta Besigye, 54, ana mke na mtoto mmoja wa

Wasifu: Osama bin Laden



Osama bin Laden, katika mojawapo ya picha enzi za uhai wake.

Siku ambayo ndege zilizotekwa nyara ziligonga majengo ya World Trade Centre na makao ya wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, ni vitendo vilivyombadilisha Osama bin Laden kutoka mtu mdogo asiyejulikana na kumfanya kuwa mojawapo watu wanaotambulikana sana duniani
Lakini alipojaribu kuepuka juhudi za Marekani kumkamata aliendelea kuwa

Kamati ya Bunge: Waziri Ngeleja, Mhando ni mzigo

23rd May 2011
Chapa
Maoni
  Yahitimisha wameshindwa majukumu yao
  Yapania kukwamisha bajeti ya Nishati
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imesema Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), William Mhando, ni mzigo kwa taifa kwa kuwa wamelidanganya Bunge, Rais Kikwete na wananchi kwa kutoa ahadi hewa kwamba mgawo wa umeme utamalizika kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.
Vile vile, Kamati hiyo imedhamiria kukwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ya mwaka wa fedha wa 2011/2012 ikiwa serikali itashindwa kutoa majibu ya uhakika kuhusu kumaliza tatizo la mgawo wa umeme nchini.
Kadhalika, Kamati hiyo imetaka majibu juu ya mapendekezo 30 iliyotoa mapema mwaka huu kwa serikali na Tanesco ili kumaliza tatizo la umeme ikiwemo kukodi mitambo ya dharura itakayokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 260.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, January Makamba aliyasema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa viongozi hao wamekuwa wakikimbilia uchochoroni kujificha badala ya kutoa majibu kuhusu ahadi zao.
“Kufuatia kauli hizo za Ngeleja na Mhando, Rais naye alilitangazia taifa hivyo hivyo kwamba ufumbuzi wa mgawo wa umeme utapatikana mwezi Juni mwaka huu jambo ambalo limeshindikana,” alisema.
Makamba alisema serikali imezoea kutoa ahadi nzito kwa

JK achangia harambee ya Chadema 10m/

23rd May 2011
Chapa
Maoni
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ameahidi kutoa Sh. Milioni 10 kwa kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya Elimu ya Jimbo la Nyamagana linaloongozwa na Mbunge Ezekia Wenje wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chandema).
Kikwete alitoa ahadi hiyo juzi usiku, katika hafla ya uzinduzi wa mfuko huo iliyofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini hapa.
Katika harambee ya kuchangia mfuko huo baada ya kuzinduliwa iliyoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, iliwezesha jimbo hilo kupata kiasi cha Sh. Milioni 50 licha ya kuhudhuriwa na watu wachache. Katika harambee hiyo, Zitto alipiga mnada sare yake iliyonunuliwa kwa Sh. milioni 1.7.
Baadhi ya vigogo wa vyama vya siasa waliopo ndani na nje ya Mkoa wa Mwanza, waliwasilisha michango yao kwa Zitto kwa sharti la kutotajwa majina yao huku Kikwete akitoa ahadi hiyo kupitia kwa Wenje.
Kikwete alitoa mchango wake huo baada ya kumpigia simu Zitto akiwa anaongoza harambee hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali, kisha kumweleza jinsi alivyoguswa na mkakati huo wa maendeleo.
Rais aliahidi kuzituma fedha hizo kwa utaratibu utakaowekwa na

Man United kumsajili kipa David de Gea

David de Gea
David de Gea

Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amethibitisha klabu hiyo inakaribia kumsajili mlinda mlango wa Atletico Madrid, David de Gea.
Manchester United inahitaji mlinda mlango wa kuchukua nafasi ya Edwin van der Sar, anayestaafu soka mwishoni mwa msimu huu.
"Tumekuwa tukilifanyia kazi suala hili la kumpata de Gea kwa muda mrefu sasa," alisema Ferguson.
"Ni kijana mdogo, mwepesi sana, anautulivu langoni na

`Nec ilichangia kuvuruga Uchaguzi Mkuu mwaka jana`

NA RICHARD MAKORE

Chapa
Maoni
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa
Kila kinapofika kipindi cha Uchaguzi Mkuu hapa nchini huwa kunaibuka mambo mengi ambayo yanahusisha wanasiasa na vyama vyao.
Wanasiasa huwa wanajitahidi kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha wanaungwa mkono na wapiga kura wao huku vyama navyo vikipiga debe ili kuhakikisha vinaibuka washindi kwa kupata Wabunge wengi, Madiwani ama Rais na hatimaye kuunda serikali.
Mwaka jana ulikuwa ni Uchaguzi Mkuu wa mara ya nne ambao ulihusisha vyama vingi tangu mfumo huo ulipoanzishwa hapa nchini mwaka 1992 ambapo vyama 18 vyenye usajili vilishiriki katika ngazi mbalimbali.
Kuna baadhi ya vyama vilisimamisha wagombea wa Urais, Ubunge na Udiwani na vipo vilivyosimamisha baadhi ya majimbo ama Kata lakini nafasi ya urais havikusimamisha mgombea.
Wiki iliyopita Vyama hivyo vya siasa na baadhi ya waliokuwa wagombea kupitia vyama hivyo walikutana ili kujadili majeraha ya Uchaguzi Mkuu uliopita ambao ulifanyika mwezi Oktoba 2010.
Katika mjadala huo, vyama hivyo vya siasa pamoja na waliokuwa wagombea wao na ambao hawakugombea nafasi yoyote mwaka jana kwa pamoja waliishutumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na

Nato yaishambulia Libya usiku kucha


Mashambulio ya anga Libya
Takriban milipuko mikubwa mitano imeitikisa Tripoli usiku kucha, wakati harakati za majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya Nato zikiendelea kwenye mji mkuu wa Libya.
Kwa usiku wa pili, mashambulio ya