Friday, 20 May 2011 08:24 |
*Wagombea Mwanamke Na Christina Gauluhanga, Temeke VURUGU kubwa ziliibuka jana baada ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mbagala kuvamia shule ya Nzasa na kuanza kuwashambulia baadhi ya wanafunzi kwa fimbo na mawe.Tukio hilo limetokea jana saa 7 mchana ambapo chanzo kikubwa inadaiwa kuwa, ni mahusiano ya kimapenzi ambapo kuna mwanafunzi wa kike mmoja alikuwa akiwachanganya wanafunzi hao wa Mbagala na Nzasa. Akizungumza na Dar Leo kwa njia ya simu, Kamanda wa |
Sunday, May 22, 2011
KIZAAZAA MBAGALA SEKONDAR IBAADA YA WANAFUNZI KUGOMBEA MWANAMKE
WANAFUNZI KIGOGO SEKONDARI WALILIA GUEST HOUSE
Friday, 20 May 2011 09:03 |
Na Masau Bwire,jijini WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Kigogo iliyopo Manispaa ya Kinondoni wamepanga kuandamana kwenda Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete kupinga kuwepo kwa nyumba ya kulala wageni bubu, ndani ya eneo la shule yao. Wamedai kuwepo kwa gesti hiyo ni kikwazo kikubwa katika masomo yao na ustawi wa maadili mema kwa watoto. Wakizungumza na Dar leo shuleni hapo jana, wanafunzi hao walisema, mbali na kuzitaarifu mamlaka husika kuhusu athari za kuwepo kwa gesti hiyo bubu ndani ya shule yao na azma yao ya |
BASENA ATAKA MECHI ZA MAJARIBIO
Friday, 20 May 2011 09:23 |
Na Mwandishi Wetu,jijini KOCHA Mkuu wa Simba Mganda Moses Basena amesema kwamba mechi moja tu ya kirafiki katika timu yake, itamsaidia kupata kikosi cha kwanza katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco, inayotarajiwa kuchezwa Mei 28 mwaka huu,jijini Cairo. Timu ya Simba imeondoka jijini leo kwenda visiwani Zanzibar kuweka kambi kwa ajili ya |
YANGA WAUNGANA NA SIMBA KLABU BINGWA AFRIKA
Friday, 20 May 2011 09:25 |
Na Elizabeth Mayemba,jijini UONGOZI wa klabu ya Yanga umewatakia kila lakheri watani zao Simba katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, baada ya kushinda rufaa yao dhidi ya TP Mazembe ya congo, baada ya kumchezesha mchezaji batili na kuwataka waitumie vizuri nafasi hiyo. Mei 28 mwaka huu, timu ya Simba inatarajiwa kucheza mchezo wake wa |
MANCHESTER CITY KUMNUNUA RONALDO KWA BILIONI 360
Friday, 20 May 2011 09:24 |
LONDON,Uingereza REAL Madrid imedaiwa kutaka kumuuza mshambuliaji wake ghari, Cristiano Ronaldo kwa klabu ya Manchester City, kwa ada itakayoweka rekodi nyingine tena ya pauni milioni 150.Awali Madrid ilimnunua mchezaji huyo kwa ya ya pauni milioni 80 kutoka Manchester United ya England misimu miwili iliyopita, ada yake iliweka rekodi ya dunia. City inataka kujiimarisha kwa kuwa msimu ujao itashiriki Ligi ya Mabingwa, na pia imeweka malengo ya kutaka kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England. Licha ya kukanushwa habari za usajili wa Ronaldo katika klabu ya City huko Eastlands, chanzo kutoka Hispania kimesema kuwa City inajaribu kufanya mazungumzo na Real kuhusu uwezekano wa kufanyika mkataba. Uhamisho huo kama utafanikiwa utatetemesha mahasimu wao Old Trafford pengine kuwakasirisha mashabiki, baada ya awali City kumchukua Carlos Tevez. Mbali ya kuweza kununulikwa kwa dau kubwa, Ronaldo anadaiwa katika mkataba wake wa miaka mitano kupangiwa kulipwa mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki ambazo ni sawa na zaidi ya sh.milioni 720 za Tanzania. Mshambuliaji huyo wa Kireno anayeongoza kwa kufunga magoli 38, akifuatiwa na Messi wa Barcelona mwenye magoli 31 katika Ligi Kuu Hispania maarufu kama La Liga, aliondoka United kutokana na kuamini kuwa anaipenda soka ya kihispania na kocha wa United Alex Ferguson alikubaliana na uhamisho wake kwa kuwa alikuwa akiondoka nje ya England. Lakini Ronaldo (26) anadaiwa kutofautikana na kocha wa Real, Mourinho na bodi ya timu hiyo inadaiwa iko tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya mchezaji wao ambaye ni hazina. |
MCHUNGAJI KKKT AVULIWA GAMBA
Friday, 20 May 2011 09:08 |
*Wachungaji wafurahia *Wajigamba wao ni maseneta Na Mwandishi wetu, Dodoma. MCHUNGAJI wa Kanisa la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Nkuhungu Victoria Ntenga, aliyeshushwa Membarani na waimbaji wawili, Medical Amon na mwenzake wakidai hawezi kulihubiria Kanisa kwa sababu si msafi, hatimaye ametolewa gamba na kuhamishiwa Makao Makuu ya Dayosisi akajitathimini, huku waumini wakionyesha na kufurahishwa na waliohama Kanisa wakiahidi kurejea. Waumini hao ambao pia wamelipongeza gazeti la Dar Leo kwa kuihabarisha jamii ukweli halisi uliojiri usharikani hapo, wamesema Ibada zilizokuwa zikikosa watu na Sadaka kushuka toka sh. |
Subscribe to:
Posts (Atom)