*Wagombea Mwanamke Na Christina Gauluhanga, Temeke
VURUGU kubwa ziliibuka jana baada ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mbagala kuvamia shule ya Nzasa na kuanza kuwashambulia baadhi ya wanafunzi kwa fimbo na mawe.Tukio hilo limetokea jana saa 7 mchana ambapo chanzo kikubwa inadaiwa
kuwa, ni mahusiano ya kimapenzi ambapo kuna mwanafunzi wa kike mmoja alikuwa akiwachanganya wanafunzi hao wa Mbagala na Nzasa.
Akizungumza na Dar Leo kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, amesema kuwa, hadi sasa jeshi lake linawashikilia wanafunzi wanne kuhusiana na vurugu hizo.
Amesema kuwa, wanafunzi wa Mbagala mmoja wao alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana ambaye pia alibaini kuwa, ana mahusiano na mwanamume mwingine anayesoma Nzasa. ambapo aliamua kwenda na kundi lake kumfanyia vurugu.
Kutokana na vurugu hizo, wanafunzi sita walipata mshtuko na walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Hata hivyo, Kamanda Missime amesema kuwa, kutokana na vurugu hizo waliokamatwa ni Shana Reagan wa kidato cha nne 'D', Twahir Sultan kidato cha tatu katika sekondari ya Nzasa, Said Muhibu mkazi wa Zakhem alijiingiza kwenye vurugu hizo na Reuben Hosea, kidato cha tatu katika sekondari ya Mbagala.
"Tumeamua kuwashikilia hawa watuhumiwa kwa kuwa wanaonekana kama ni wahuni na si wanafunzi kwani wamewezaje kujiingiza kugombea mwanamke wakati bado wapo shuleni, hivyo tukijiridhisha tutawafikisha Mahakamani," amesema Kamanda Missime.
Kamanda Missime amesema kuwa, jeshi lake linaendelea na upelelezi na litawafikisha mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
|
No comments:
Post a Comment