Send to a friend |
Friday, 12 August 2011 21:43 |
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), imesitisha leseni ya biashara ya Kampuni ya Mafuta ya BP kwa miezi mitatu kwa kukaidi agizo lake la kutoa huduma ya uuzaji wa mafuta.Imesema Bodi yake ya Wakurugenzi imeagiza Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa kampuni hiyo pekee ya mafuta ambayo Serikali ina hisa asilimia 49, afikishwe mahakamani kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP) kwa kukaidi agizo hilo la Ewura. Pia, imezipa onyo kali Kampuni za Oilcom, Camel Oil na Engen na kuzitaka kutorudia tabia ya kugoma kupunguza bei ya mafuta kwa kuwa ni kinyume na sheria za Tanzania, huku ikiwataka kuuza mafuta kama awali kwa watu wote bila ubaguzi.Rungu hilo la Ewura linakuja takriban wiki moja baada ya wafanyabiashara wa mafuta kugoma kuuza nishati hiyo kwa bei elekezi ya Serikali. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa |