Siku 13 tangu tuhuma hizo zirushwe bungeni, Kikwete amekaa kimya. Hata waziri mkuu, Mizengo Pinda aliyedaiwa kujibu tuhuma hizo wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu makadirio ya wizara yake, “aliishia kudodosa tu,” wachambuzi wa siasa wanasema.
Edward Lowassa, waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashifa ya Richmond, alimshukia Kikwete na