Thursday, July 14, 2011

Sneijder mbioni kutua Man United.


Wednesday, 13 July 2011 20:05
0diggsdigg
LONDON, England
MANCHESTER United ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa pauni 35milioni wa Wesley Sneijder jana usiku kama lilivyoripoti SunSport.

Mkurugenzi wa United, David Gill yuko nchini Italia kwa lengo la kufanikisha uhamisho wa kiungo huyo wa Inter Milan. Gill amekwenda kwa niaba ya Manchester ili kufanikisha uhamisho huo wakati Alex Ferguson na kikosi chote cha timu hiyo wakiwa nchini Marekani.

Utakuwa usajili mkubwa kwa Ferguson, ambaye kwa sasa anataka kutumia zaidi ya pauni 85m kwa ajili ya usajili wa wachezaji wanne aliowanunua hadi sasa Phil Jones, Ashley Young na  kipa David De Gea.

Kila wakati amekuwa akitaka kutafuta mchezaji ambaye atakuwa na uwezo wa kuziba pengo la Paul Scholes hivyo anaamini Sneijder ndiye mwenye uwezo huo.

Nahodha wa zamani wa United, Gary Neville alisema: "Sneijder ni mchezaji mwenye akili ya soka." Ferguson amekili mrithi wa Scholes ni lazima awe mchezaji wa kiwango cha juu duniani.

Fergie alisema: "Unapotaka kutafuta mrithi wa Scholes ni lazima kupata mchezaji wa kiwango cha juu mwenye uwezo wa kuchezesha timu kama  Xavi na Andres Iniesta, huyo ndiye mchezaji ninayemtafuta.
venance.chadema@yahoo.com

No comments:

Post a Comment