Monday, July 18, 2011

Chadema wamuundia tume John Shibuda .

venance.chadema@yahoo.com
 
Monday, 18 July 2011 21:34


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeunda tume itakayoongozwa na Profesa Abdallah Safari kumhoji Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu zinazomkabili.

Hii ni mara ya pili kwa Shibuda kuhojiwa na jopo maalumu la Chadema kwani tayari aliwahi kuhojiwa baada ya kupingana na msimamo wa chama hicho wa kumsusia Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akizundua Bunge Desemba mwaka jana kwa kuhudhuria dhifa katika Ikulu ya Chamwino huku akiweka bayana kupingana na msimamo huo.

Mapema mwezi huu alitoa tena kauli ambazo Chadema imeziita ni

Shellukindo ailipua Wizara ya Ngeleja .

venance.chadema@yahoo.com

Monday, 18 July 2011 21:36
MBUNGE wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo amelipua bomu Bungeni akimtuhumu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, kwa kutumia zaidi ya Sh 1 bilioni kwa ajili ya kutoa rushwa kwa watu mbalimbali ili bajeti ya wizara hiyo iweze kupitishwa na Bunge.Tuhuma hizo nzito zinakuja kipindi ambacho tayari Wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini wakiwa wameibua tuhuma kama hizo za baadhi ya wajumbe kutaka kuhongwa na maofisa wa wizara hiyo, ili kurahisisha upitishaji wa bajeti ndani ya kamati.

Takriban wiki tatu tangu wabunge wa kamati hiyo kuibua tuhuma