Sunday, May 22, 2011

MCHUNGAJI KKKT AVULIWA GAMBA

Friday, 20 May 2011 09:08
*Wachungaji wafurahia
*Wajigamba wao ni maseneta

Na Mwandishi wetu, Dodoma.
MCHUNGAJI wa Kanisa la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Nkuhungu Victoria Ntenga, aliyeshushwa Membarani na waimbaji wawili, Medical Amon na mwenzake wakidai hawezi kulihubiria Kanisa kwa sababu si msafi, hatimaye ametolewa gamba na kuhamishiwa Makao Makuu ya Dayosisi akajitathimini, huku waumini wakionyesha na kufurahishwa na waliohama Kanisa wakiahidi kurejea.

Waumini hao ambao pia wamelipongeza gazeti la Dar Leo kwa kuihabarisha jamii ukweli halisi uliojiri usharikani hapo, wamesema Ibada
zilizokuwa zikikosa watu na Sadaka kushuka toka sh.
milioni moja hadi laki tatu kwa kukerwa, sasa zitaongezeka mara dufu.

Habari za Uhakika toka vyanzo vyetu vya ndani ya kikao cha maamuzi yaliyofikiwa mwanzoni mwa wiki, zimelifikia Dar Leo kuhusu kuhamishwa kwa mchungaji kwenda Makao Makuu ya Dayosisi ili nafasi itwaliwe na mchungaji mwingine, jambo lililowafurahisha waumini hata wale waliohama kanisa na kuahidi kurejea mara
moja.

“Naupongeza uongozi wa KKKT kwa maamuzi iliyoyafanya, na pia ninalishukuru Dar Leo, na watendaji wa Radio Clouds FM, kwa kuihabarisha jamii,
ili isifikirie ndani ya madhehenu kuna amani, Mmteremko na uchaji, nasema kama ilivyo nje ya madhehebu, ndani mwake kuna vitu vya ajabu hata uchawi,” alisema mmoja akiomba asitajwe.

Mchungaji Ntenga ambaye awali alipozungumza na Dar Leo, aliwadharau waliodiriki kumshusha membarani kuwa, hawana akili timamu, baada ya maamuzi ya uongozi kumhamisha, atakuwa alifuta usemi wa sintofahamu na kuamini vijana wawili waliodiriki kumshusha, walikuwa na akili timamu na yenye mtazamo wa kiroho.

Wachungaji waliojigamba na kujiita Maseneta kutokana na kukataliwa na waunini kila wanapohamishiwa, hawakufurahishwa na maamuzi yaliyofikiwa, ingawa wenye msimamo mkali wa kiroho walioomba wasitajwe walisema, KKKT na Dayosisi
zitakuwa matatani zisipokuwa makini na tabia ya kila Mchungaji au Mtumishi anapotuhumiwa arudishwe Dayosisi, kwamba dhana hiyo baadaye itapafanya kuwa Kapu la kutunzia wenye maovu, hivyo wawajibishwe.
 

No comments:

Post a Comment