Sunday, May 22, 2011

MANCHESTER CITY KUMNUNUA RONALDO KWA BILIONI 360

Friday, 20 May 2011 09:24
LONDON,Uingereza

REAL Madrid imedaiwa kutaka kumuuza mshambuliaji wake ghari, Cristiano Ronaldo  kwa klabu ya Manchester City,  kwa ada itakayoweka rekodi nyingine tena ya pauni milioni 150.Awali Madrid ilimnunua mchezaji huyo kwa ya ya pauni milioni 80 kutoka Manchester United ya England misimu miwili iliyopita, ada yake iliweka rekodi ya dunia.

City inataka kujiimarisha kwa kuwa msimu ujao itashiriki Ligi ya Mabingwa, na pia imeweka malengo ya kutaka kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Licha ya kukanushwa habari za usajili wa Ronaldo katika klabu ya City huko Eastlands, chanzo kutoka Hispania kimesema kuwa City inajaribu kufanya mazungumzo na Real kuhusu uwezekano wa kufanyika mkataba.

Uhamisho huo kama utafanikiwa utatetemesha mahasimu wao  Old Trafford pengine kuwakasirisha mashabiki, baada ya awali City kumchukua Carlos Tevez.

Mbali ya kuweza kununulikwa kwa dau kubwa, Ronaldo anadaiwa katika mkataba wake wa miaka mitano kupangiwa kulipwa mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki  ambazo ni sawa na zaidi ya sh.milioni 720 za Tanzania.

Mshambuliaji huyo  wa Kireno anayeongoza kwa kufunga magoli 38, akifuatiwa na Messi wa Barcelona mwenye magoli 31 katika Ligi Kuu Hispania maarufu kama La Liga, aliondoka United kutokana na kuamini kuwa anaipenda soka ya kihispania na kocha wa United Alex Ferguson alikubaliana na uhamisho wake kwa kuwa alikuwa akiondoka nje ya England.

Lakini Ronaldo (26) anadaiwa kutofautikana na kocha wa
Real, Mourinho na bodi ya timu hiyo inadaiwa iko tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya mchezaji wao ambaye ni hazina.

No comments:

Post a Comment