Saturday, June 25, 2011

Tusker All stars ni kesho!



Saturday, 25 June 2011 15:02
Na Henry Mdimu
Msimu wa tano wa Shindano uimbaji Tusker project fame ambacho ni moja kati ya vipindi maarufu kabisa vya televisheni Afrika, unatarajiwa kuzinduliwa kesho majira ya saa moja na nusu usiku na kwa Tanzania mashabiki wa shoo hiyo inayoteka mashabiki lukuki Afrika ya Mashariki wataiona moja kwa moja kupitia kituo cha televisheni cha taifa TBC1, Kenya wataona kupitia Citizen TV na Uganda wataona kupitia UBC.
safari hii imeitwa Tusker all stars kwa sababu imechukua washiriki mbali mbali kutoka mashindano yaliyopita ambao waliwahi nkuwa maarufu na kuwaweka katika jumba moja kwa takriban wiki nane

Mahita 'aangukia pabaya' kortini.

 
Saturday, 25 June 2011 09:44
James Magai

MKUU wa zamani wa Jeshi la Polisi Nchini, Omar Mahita, ameumbuka kwa mara nyingine baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kutupilia mbali rufaa yake ya kupinga hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, kuhusu sakata la mtoto anayemkataa.

Rufaa hiyo ya Mahita ilitupiliwa mbali jana na Jaji Dk Fauz Twaib, baada ya kuridhika na hukumu ya mahakama ya chini kuwa ilikuwa sahihi na kumwamuru Mahita kulipa gharama za kesi hiyo.

Hata hivyo wakati hukumu hiyo ikitolewa, Mahita hakuwapo mahakamani na wakili wake Semgalawe, alifika wakati tayari jajiakiwa ameshamaliza kusoma hukumu.
 Septemba mwaka 2009 Mahakama ya Kinondoni  ilimwamuru Mahita kutoa kiasi cha Sh100,000 kila mwezi kwa ajili ya

Mrema aidai serikali mafao ya ubosi wake

 
Saturday, 25 June 2011 10:04
Kizitto Noya, Dodoma
MWENYEKITI wa TLP Augustine Mrema, ametoa mpya bungeni kufuatia hatua ya kuidai serikali mafao ya kutumikia nafasi ya Naibu waziri mkuu.Akichangia mjadala wa hotuba ya Waziri Mkuu jana bungeni, Mrema aliitaka serikali impe mafao yake ya kutumikia  nafasi ya Naibu Waziri Mkuu wakati wa Serikali ya Awamu ya Pili.

Katika mchango wake, Mrema aliitaka serikali imlipe angalau asilimia 20, kama serikali inaona hastahili.Katika kipindi hicho, Mrema alikuwa Naibu Waziri Mkuu akimsaidia John Malecela ambaye ndiye aliyekuwa Waziri Mkuu.
"Kama Sheria ipo kwamba Waziri mkuu mstaafu anatakiwa kulipwa mafao ya asimilia 80 ya mshahara wa waziri mkuu aliyeko madarakani, kwanini mimi sipati. Nipeni basi angalau asilimia 20,"alisema Mrema na kuendelea:

 "Nilipeni posho hiyo ili niendelee kuwatetea (serikali) bungeni. Msione simba kalowa maji mkadhani nyani. Mimi najua mambo mengi nchi hii, mmenifundisha wenyewe. Nipeni haki yangu niwasaidie kutetea hoja zetu hapa bungeni," alisema.

 Mrema aliendelea kuhoji imekuaje mawaziri wakuu wote wastaafu walipwe posho hiyo na

Mbunge aanguka,azirai bungeni.


 
Saturday, 25 June 2011 10:09
Kizitto Noya na Habel Chidawali, Dodoma
TAHARUKI kubwa ililikumba Bunge jana kuanzia ukumbini hadi nje baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Mwanakhamis Kassim Said (CCM) kuanguka ghafla na kuzirai.

Tukio hilo lilitokea saa 6:10 mchana wakati wabunge wakiendelea  na mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2011/2012.

Mbunge huyo alianguka kutoka kwenye kiti chake na kisha kuzungukwa na wabunge wengi ambao walianza kumpa huduma ya kwanza. Wakati huo, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM) alikuwa akichangia hotuba hiyo.

Mwenyekiti wa Bunge, Sylvester Mabumba kama ilivyokuwa kwa wabunge wengine wengi alionekana kushangazwa na tukio hilo.Takribani, robo ya wabunge wote waliokuwamo ukumbini humo waliinuka vitini na

LOWASA AILAUMU SERIKALI YA JAKAYA, ASEMA INAOGOPA KUFANYA MAAMUZI MAZITO.



Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akichangia bungeni, makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2011/2012, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi


Kizitto Noya, Dodoma
MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa ameiambia Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwa inasumbuliwa na ugonjwa wa woga katika kutoa uamuzi magumu na matokeo yake mambo yake mengi hayaendi kama yalivyopangwa.Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza katika utawala huu wa awamu ya nne, pia akaitaka Serikali hiyo kubadilika.

Alisema kuwa ni bora kulaumiwa kwa kufanya uamuzi mgumu kuliko kulaumiwa kwa kutofanya uamuzi na kwamba Serikali inapaswa kufanya maamuzi bila kujali matokeo yake huku akipendekeza kwa kuanzia, ikope kwa kutumia rasilmali za nchi.

Alitoa kauli hiyo wakati akichangia hotuba ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka 2011/2012.
"Ni bora kulaumiwa kwa kufanya maamuzi kuliko kulaumiwa kwa kutofanya maamuzi kabisa,"alisema Lowassa.

Bila kueleza ni maamuzi gani ambayo serikali hiyo imeshindwa kufanya, Lowassa alisema ugonjwa wa viongozi kuogopa kufanya maamuzi ni hatari kwa uchumi wa taifa kwa kuwa kuthubutu ni msingi wa mafanikio katika nyanja mbalimbali kijamii na kiuchumi.

"Kuna ugonjwa wa kutokutoa maamuzi hapa na lazima tukubali kubadilike. Ni heri mtu ukosee kutoa maamuzi kuliko kukaa kimya kabisa, heri uhukumiwe kwa kutoa maamuzi kuliko ulaumiwe kwa kushindwa kutoa maamuzi,"alisema.

Lowassa alitoa kauli hiyo huku serikali ikionekana kushindwa kutatua matatizo mbalimbali yaliyoko nchini hivi