Saturday, 25 June 2011 15:02 |
0digg Na Henry MdimuMsimu wa tano wa Shindano uimbaji Tusker project fame ambacho ni moja kati ya vipindi maarufu kabisa vya televisheni Afrika, unatarajiwa kuzinduliwa kesho majira ya saa moja na nusu usiku na kwa Tanzania mashabiki wa shoo hiyo inayoteka mashabiki lukuki Afrika ya Mashariki wataiona moja kwa moja kupitia kituo cha televisheni cha taifa TBC1, Kenya wataona kupitia Citizen TV na Uganda wataona kupitia UBC. safari hii imeitwa Tusker all stars kwa sababu imechukua washiriki mbali mbali kutoka mashindano yaliyopita ambao waliwahi nkuwa maarufu na kuwaweka katika jumba moja kwa takriban wiki nane na mwisho wa yote watakuja kumpata supastaa wa Tusker ambaye atakuwa mwanamuziki haswa, kwa mujibu wa waandaaji. Mastaa nane wanatarajiwa kuongozwa na watayarishaji wanne maarufu wa muzikii katika kuhakikisha kwamba wanakuwa wanamuziki bora pindi watakapotoka katika jumba hilo, hii ikiwa ni hapo baada ya wiki nane za kuisha kwa pambano hilo la kukata na shoka ambalo linatarajiwa kupiga nanga itakapofika mwezi Agosti mwaka huu. Kwa Tanzania tutawakilishwa na Hemed Suleyman na Petter Msechu, davies kutoka Uganda ambaye ni mshindi wa mwaka jana pia amerudi, Alpha naye ndani, mtu mzima Ngangalito karudi pia pamoja na mwanadada Amileena, Patricia na Carolina. washiriki hawa ambao ni mastaa utoka katika nchi zao wataongozwa na wataalam wanne wa muziki ambao ni Tim Rimbui ambaye ni mhandisi wa Sauti, Victor Sei ambaye ni mwanamuziki mahiri wa jazz, Chris Adwar ambaye ana vipaji lukuki vya sanaa ya muziki wa jukwaani na Aaron Rimbui ambaye pia ni mkali wa muziki wa Jazz. Katika msisimko mwingine ambao utaletwa na shoo ya msimu huu wa mastaa, staa kutoka Uganda ambaye aliwahi kuwa gumzo la shindano la Big Brother Africa msimu wa kwanza, Gaetano Kagwa ndio atakuwa mtangazaji wa kiume, huku akisaidiwa kwa ukaribu kabisa na Eve D'Souza. Kitu kingine kikubwa ambacho kitakuwa tofauti na nchi nyingine ambazo ni mashabiki, ni kwamba nchi ya Rwanda, ndiyo pekee ambayo haitakuwa ikipata shindano hili moja kwa moja, itakuwa ikiliona Jumatatu lakini kwa wateja wa DSTV watakuwa wakiona kupitia chaneli za TBC na Citizen TV. |
No comments:
Post a Comment