Friday, July 15, 2011
LAPF yaongeza uwekezaji hadi sh. bilioni 265.9
venance.chadema@yahoo.com
MFUKO wa Pensheni kwa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF) umeongeza uwekezaji kutoka sh. bilioni 154.5 kuanzia Juni 2008 hadi kufikia sh.bilioni 265.9 ilipofika
Juni mwaka huu.
Akizungumza katika Mkutano na Ujumbe Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)na balozi mdogo wa Kenya nchini Kenya, aliyetaka kujua muundo wa mfuko huo, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji LAPF, Bi, Rose Metta, alisema uwekezaji umezidi kukua kwa asilimia 106.
Akieleza upatikanaji wa fedha hizo,
Bi. Metta alisema zinatoka kwenye michango ya wanachama, mapato
Juni mwaka huu.
Akizungumza katika Mkutano na Ujumbe Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)na balozi mdogo wa Kenya nchini Kenya, aliyetaka kujua muundo wa mfuko huo, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji LAPF, Bi, Rose Metta, alisema uwekezaji umezidi kukua kwa asilimia 106.
Akieleza upatikanaji wa fedha hizo,
Bi. Metta alisema zinatoka kwenye michango ya wanachama, mapato
Uhuru:Tujenge timu, hakuna aliyehongwa.
Thursday, 14 July 2011 22:19 |
WINGA wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba, Uhuru Selemani amewasihi mashabiki na viongozi wa timu hiyo kuacha tabia ya kuwahukumu wachezaji kwamba walihujumu na kufungwa na wapinzani wao Yanga bao 1-0 kwenye fainali ya Kombe la Kagame iliyofanyika Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kauli ya nyota huyo ambaye hivi karibuni amerejea dimbani baada ya kupona goti lililokuwa linamsumbua inafuatia kitendo cha baadhi ya mashabiki wa Simba kuwatuhumu baadhi ya wachezaji kuwa ndio sababu ya timu yao kufungwa na Yanga siku ya fainali. Wachezaji wa Simba wanaoshutumiwa na mashabiki kuwa walifanya hujuma na kuchangia timu hiyo kufanya vibaya ni kiungo Mohamed Banka, mshambuliaji Musa Hassan Mgosi na beki Kelvin Yondani. Simba ilikuwa haipewi hata nafasi ya kufika kwenye raundi ya pili kutokana na kuwa na kikosi dhaifu baada ya kutimua nyota wake wengi siku chake kabla ya michuano hiyo, lakini wachezaji hao waliweza kupigana na kufika fainali. Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana Uhuru alisema |
Tanesco waingiza mitambo ya kufulia umeme.
Thursday, 14 July 2011 22:12 |
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limeanza kuingiza mitambo yenye thamani ya Dola 120 milioni za Marekani kwa ajili ya kufulia umeme, katika Mkoa wa Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Meneja Mahusiano kwa Umma katika Tanesco, Badra Masoud, mitambo hiyo itatumia gesi asilia kuzalishia umeme kwa kiwango cha megawati 100. Alisema kwa sasa shirika lina upungufu wa megawati 250 za umeme yakiwa ni matokeo ya kupungua kwa kina cha maji katika Mabwawa ya Kidatu na Mtera. Badra ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alisema tayari shirika limeshaingiza mtambo mmoja na mingine miwili itaingia wakati wowote kuanzia sasa. Pia alisema kiwango cha mgawo wa umeme kimeongezeka kwa saa 18 badala ya 12 na kwamba hiyo inatokana na sababu za kitaalamu, zilizolilazimisha shirika kuzima mitambo ya uzalishaji. "Wananchi wamekosa imani na Tanesco hata wanapotuona hii ni kutokana na |
Washtakiwa 31 ‘samaki wa Magufuli’ waachiwa.
Send to a friend |
Thursday, 14 July 2011 22:25 |
JUMLA ya washtakiwa 31 kati ya 36 waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uvuvi haramu katika Ukanda wa Kiuchumi wa Tanzania maarufu kama kesi ya samaki wa Magufuli wameachiwa huru. Washtakiwa hao kutoka Mataifa ya China, Ufilipino, Vietnam na Kenya walikuwa wakituhumiwa kufanya shughuli za uvuvi katika eneo hilo bila kuwa na kibali na kuchafua mazingira ya bahari katika eneo hilo. Lakini jana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaa mbele ya Jaji Augustine Mwarija anayesikiliza kesi hiyo iliwaachia huru washtakiwa hao baada ya kuridhika kuwa hawana kesi ya kujibu kuhusiana na tuhuma zilizokuwa zikiwakabili. Wakati wakiachiwa huru jana washtakiwa hao walikuwa wameshasota mahabusu kwa muda wa miaka miwili na miezi minne tangu walipokamatwa Machi 9 hadi walipoachiwa huru jana.Wakati 31 wakiachiwa huru kwa kutokuwa na kesi ya kujibu washtakaiwa wengine watano wamepatikana na kesi ya kujibu na hivyo mahakama kuwataka wajitetee kuhusiana na tuhuma hizo. Waliopatikana na kesi ya kujibu ni pamoja na mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo Hsu Chin Tai ambaye ni Nahodha wa meli waliyokuwa wakiitumia kwa shughuli za uvuvi. Wengine ni mshtakiwa wa saba Zhao Hanquing, mshtakiwa wa tisa Hsu Sheng Pao ambao wote ni mawakala wa meli hiyo, pamoja na wahandisi wawili wa meli hiyo Cai Dong Li mshtakiwa wa 33 na Chen Rui Hai mshtakiwa wa 34. Akisoma uamuzi wake jana Jaji Mwarija alisema kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka hususani ushahidi wa shahidi wa tatu Nahodha Ernest Bupamba kutoka Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi ameridhika kuwa washtakiwa hao wana kesi ya kujibu. Bupamba ambaye ni Ofisa msimamizi wa sheria na shughuli za uvuvi katika ushahidi wake aliieleza mahakama kuwa ndiye aliyewakamata wakati wakifanya doria na timu ya wanadoria kutoka mataifa matatu. Mbali na ushahidi wake wa mdomo kuwa rada aliposoma kwenye rada iliyokuwa kwenye meli yao ya doria ilionyesha kuwa walikuwa katika eneo la Tanzania, pia Nahodha Bupamba aliwasilisha mahakamani vielelezo huku akiwasilisha mahakamani vilelezo vya picha zinazohusiana na mashtaka hayo. Tai (nahodha), Li na Hai (wahandisi) wakipatikana na kesi ya kujibu katika kosa la kwanza la kufanya shughuli za uvuvi katika Ukanda wa Bahari Kuu ya Tanzania bila kuwa leseni na kosa la pili la kuchafua mazingira ya bahari kwa uchafu wa samaki na mafuta ya meli. Kwa upande wao Hanquine na Pao (mawakala) wao walipatikana na kesi ya kujibu katika kosa la tatu ambalo ni kosa mbadala wa kosa la kwanza na la pili, yaani kosa la kutaka kuwasaidia washtakiwa wengine wakwepe mashtaka(Accessory after the fact). Katika shtaka hilo la tatu washtakiwa hao wanatuhumiwa kuwa baada ya washtakiwa wengine kukamatwa washtakiwa hao walifika nchini wakiwa na leseni na hati za meli ili kuonyesha kuwa walikuwa wakifanya shughuli za uvuvi kihali ili wapone katika mashtaka hayo. Kabla ya kuwaachia hao 31 na kuwakuta na kesi ya kujibu watano kwanza Jaji Mwarija alianza kwa kurejea majumuisho ya hoja za pande zote na kuanza kuchambua moja baada ya nyingine, huku akitupilia mbali na kukubaliana na baadhi ya hoja za pande hizo zote. Baada ya kufanya uchambuzi wa hoja hizo Jaji Mwarija alisema kuwa ameridhika kuwa kwa jinsi inavyoonekana kutokana na ushahidi uliopo upande wa mashtaka umethibitisha kesi katika shtaka la kwanza na pili. “Lakini swali la kujiuliza ni kwamba ni kwa nani upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha kesi katika makosa hayo,” alijihoji Jaji Mwarija.Alisema hakubaliani na upande wa mashtaka kuwa umethibitisha kesi katika mashtaka hayo kwa kila mshtakiwa. Aliongeza kuwa ushahidi wa washtakwa wote kukutwa tu ndani ya meli hautoshi kwani majukumu ya kila mmoja katika meli hayakuwekwa wazi na kwamba upande wa mashtaka ulipaswa kuliweka wazi, kwani si kweli kwamba wote walikuwa wakivua samaki. “Kigezo katika shtaka la kwanza ni kuvua bila kuwa na leseni. Lakini kuna ushahidi kwamba wengine walikuwa ni wapishi ndani ya meli ile,” alisema Jaji Mwarija na kuongeza kuwa kwa mujibu wa shahidi wa sita (PW6) suala la leseni ni jukumu la nahodha. |
Mchumba wa Slaa avamiwa, aporwa.
Thursday, 14 July 2011 22:27 |
JOSEPHINE Mushumbushi, ambaye ni mchumba wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa, amevamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na kuporwa simu mbili, kamera na fedha taslimu sh 50,000. Tukio hilo ambalo lilitokea jijini Dares Salaam juzi, karibu na SUMA-JK, ni mwendelezo wa wimbi la matukio ya uhalifu wa kutumia pikipiki maarufu kama bodaboda. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alifafanua kwamba tukio hilo lilitokea juzi mnamo saa 11:57 jioni, wakati Mushumbushi akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Harrier lenye |
Lowassa: Nimeshtushwa.
Send to a friend |
Thursday, 14 July 2011 22:42 |
WAKATI uamuzi wa Rostam Aziz kung'atuka ubunge wa Igunga na ujumbe wa Halmashauri Kuu (Nec) ndani ya chama chake cha CCM ukiibua gumzo kubwa karibu kila kona nchini, mshirika wake mkubwa kisiasa, Edward Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli ameeleza kushtushwa na tukio hilo.Juzi, Rostam, mmoja wa watu muhimu ndani ya CCM aliyeshiriki vyema katika mtandao uliomwingiza madarakani Rais Jakaya Kikwete mwaka 2005, alitangaza uamuzi mzito wa kung'atuka siasa akipinga kile alichokiita siasa uchwara za baadhi ya viongozi wake.Uamuzi huo mzito wa Rostam uliibua kwikwi na vilio kutoka kwa wapigakura jimboni kwake Igunga, wakiwamo wale waliomchagua kwa vipindi vitatu mfululizo tangu mwaka 1994 ulipofanyika uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Charles Kabeho. Jana, Lowassa alisema: "Kwa kweli nimeshtushwa, nimesikitishwa...kilichonishtua zaidi ni vilio. Namna wananchi wa Igunga walivyokuwa wanalia na kusikitika." Hata hivyo, Lowassa ambaye naye amekuwa akitajwa katika orodha ya |
Subscribe to:
Posts (Atom)