Juni mwaka huu.
Akizungumza katika Mkutano na Ujumbe Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)na balozi mdogo wa Kenya nchini Kenya, aliyetaka kujua muundo wa mfuko huo, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji LAPF, Bi, Rose Metta, alisema uwekezaji umezidi kukua kwa asilimia 106.
Akieleza upatikanaji wa fedha hizo,
Bi. Metta alisema zinatoka kwenye michango ya wanachama, mapato kutoka katika uwekezaji wa mfuko, uwekezaji uliokomaa na ruzuku na mikopo.
Hata hivyo alisema hadi sasa mfuko huo umefanikiwa kuwekeza katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Alitaja maeneo hayo kuwa ni Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Chuo
cha Serikali za Mitaa cha Hombolo Dodoma, Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson
Mandela Arusha,Kituo cha Mabasi cha Msamvu Morogoro ,Kituo cha mabasi cha Ubungo na
Mbezi Louis.
Uwekezaji huo ni katika jengo la millennium Tower jijini Dar es Salaam na Mwanza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa Mfuko huo, Bi. Bw Valerian Mablangeti, alisema hadi Juni 2011, Mfuko ulifanikiwa kufikisha wanachama 80,000 ambao wameongeza makusanyo ya fedha kutoka sh. bilioni 151.8 mwaka 2005-2006 hadi kufikia sh. Bilioni 361.9 mwaka 2011.
Alibainisha kwamba pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto ambazo wanakabiliana nazo.Changamoto hizo ni pamoja na kuchelewa kwa michango ya wanachama kutoka halmashauri.
Alisema kipindi cha nyuma halmashauri zilikuwa zikidaiwa fedha nyingi lakini zimelipa na zinaendelea kulipa madeni hayo.
Ujumbe uliotembelea mfuko huo na miradi yake ya uwekezaji ni Meneja Mkuu wa NSSF
Kenya Bw. Tom Odongo na Balozi Mdogo wa Kenya Bw, Patrick Nzusi.
No comments:
Post a Comment