' | Send to a friend |
Wednesday, 13 July 2011 20:50 |
0diggsdigg Leon Bahati, DodomaMBUNGE wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed amesema Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, amewadhalilisha viongozi makini wa upinzani kufuatia kauli yake kuwa wabunge wa upinzani ni wanafiki. Kwa mujibu wa Mohamed viongozi ambao Sitta amewadhalilisha ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipimba. Hamad alitoa dukuduku hilo jana baada ya kuomba mwongozo wa Naibu Spika, Job Ndugai kuhusu kauli hiyo ilitolewa juzi na kumalizika wakati wabunge kadhaa wa kambi ya upinzani wakisimama ama kutoa taarifa au kuomba mwongozo. Hamad alisema katika vyama vya upinzani, kuna viongozi wengi makini kama vile Maalim Seif na Profesa Lipumba na kwamba kitendo cha Sitta kudai kuwa kambi ya upinzani ina wanafiki, kimewadhalilisha viongozi hao."Kauli ya jana inafanya tuonekane hovyo hovyo, naomba Bunge litoe kauli ambayo itaweka wazi suala hilo," alilalamika Hamad.Hata hivyo, Ndugai alisema tayari suala hilo lilishatolewa uamuzi na mamlaka ya spika na kwa hiyo, halina nafasi ya kujadiliwa tena ndani ya Bunge. "Hatuwezi kuibua tena suala ambalo tayari nimeshalitolewa uamuzi," alisema Ndugai na kufutilia mbali hoja ya Hamad ambaye wakati huo alionekana kutabasamu na kutikisa kichwa akiashiria kupokea jibu hilo.Ndugai alikuwa amekwishatolea suala hilo uamuzi wakati akijibu ombi la mwongozo lililotolewa na Mchungaji Peter Msigwa, (Iringa Mjini-Chadema).Mchungaji Msigwa alisema wakati Sitta akitoa kuhusu zogo lililotokea baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila (Chadema), kuitaja serikali kuwa ni legelege na inashindwa kukusanya kodi,aliwaita wabunge wa upinzani kuwa ni wanafiki hasa kwa kauli zao za kutaka posho ya wabunge iondolewe. Msigwa alifafanua kuwa suala la kukataa posho limo ndani ya sera za Chadema na kwamba kitendo cha Sitta kuwaita wanafiki, ni kauli ya kuudhi.Alimtaka Ndugai kutumia mamlaka yake, kumwamuru Sitta ambaye anakaimu nafasi ya kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, athibitishe au akanushe kauli hiyo.Waziri huyo amekuwa akikaimu nafasi hiyo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye alikuwa ziarani, Korea Kusini Hata hivyo, Ndugai hakutoa nafasi kwa Sitta kujibu hoja hiyo na badala yake, aliamua kumtetea akitoa tafsiri halisi ya kauli aliyoitoa.Ndugai alianza kujenga hoja kwa kurejea katika kauli iliyochochea Sitta kutoa dukuduku hilo ya Kafulila ambaye alisema wabunge ni kundi ambalo limependelewa kwa nafasi ya kuweza kupata huduma bora za afya ikilinganishwa na mengine. Lakini, Ndugai alipinga kauli hiyo na kusisitiza kuwa si ya kweli kwa sababu hakuna hata mmoja mwenye bima ya afya.Alisema Tume ya Huduma za Bunge, ipo kwenye mkakakti wa kuwezesha wabunge kuwa na bima ya afya.Kuhusu kauli ya Sitta, alisema hoja yake ilizingatia Bunge lililopita ambapo baadhi ya wabunge wanaolalamika wakitaka posho ziondolewe, walikuwa wakizichukua bila wasiwasi. Lakini alisema kinachoshangaza ni jinsi wanavyokuwa na msimamo kwamba sasa ziondolewe na kwamba kama siyo unafiki, basi wangerejesha zile walizochukua miaka mitano iliyopita.Kauli hiyo, iliwafanya wabunge wa kambi ya upinzani, kuelezea kutoridhishwa kwao na majibu hao na kutaka wapewe nafasi ili watoe taarifa. Hata hivyo Naibu spika aliahirishe Bunge huku kelele za wabunge zikiwa zionavuma kwenye vipaza sauti wakisisitiza wapewe nafasi ya kutoa taarifa au kuomba mwongozo.Wakati akitoa taarifa , Sitta aliwataka wabunge wa CCM wasiendelee kubishana na wabunge wa kambi ya upinzani kwa sababu ambao alisema wamekuwa wakitoa maneno ya kuudhi dhidi ya serikali. |
No comments:
Post a Comment