Showing posts with label MREMA VENNCE. Show all posts
Showing posts with label MREMA VENNCE. Show all posts

Thursday, June 23, 2011

JAJI WEREM ACHAFUA HLI YA HEWA BUNGENI.

 Send to a friend
Wednesday, 22 June 2011 22:00

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema
Kizitto Noya, Dodoma
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema jana alijikuta kwenye mgogoro na wabunge baada ya kueleza bungeni kuwa baadhi yao wanazungumza bila kufikiri ili waonekane kwenye luninga.

Tukio hilo lilitokea jana wakati Bunge limekaa kama kamati kupitisha Muswada wa Fedha wa mwaka 2011 ulioletwa bungeni kwa mara ya pili na Naibu wa Waziri wa Fedha na Uchumi, Pereira Silima .

Chanzo cha mgogoro huo ni mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuleta mapendekezo katika kifungo cha tano cha Muswada huo kutaka Kamishna na watendaji wa Serikali kuondolewa madaraka ya kusamehe kodi.

Lissu alilieleza Bunge kuwa tabia hiyo ndiyo mwanzo wa rushwa na ufisadi nchini kwani baadhi ya watendaji hao wamekuwa wakitumia vibaya mamlaka hizo. Lissu alitaka anayekosea katika suala la kodi akutane na adhabu.

Baada ya mapendekezo hayo, Mwenyekiti Anne Makinda alimtaka Mwanasheria Mkuu wa