Showing posts with label Dodoma na Furaha Maugo. Show all posts
Showing posts with label Dodoma na Furaha Maugo. Show all posts

Wednesday, August 17, 2011

Tibaijuka awatisha Malecela, Sumaye, AONYA MUDA WAO KUHODHI ARDHI KUBWA UMEKWISHA

venance.chadema@yahoo.com

Tuesday, 16 August 2011 23:34


Waandishi wetu, Dodoma, Dar
LICHA ya kupata wakati mgumu Bungeni, Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imepitishwa jana huku Waziri wake, Profesa Anna Tibaijuka akitoa onyo kwa wanaohodhi ardhi kwa muda mrefu bila kuiendeleza akisema: “Fungate yao imekwisha.”

Kauli hiyo ya Profesa Tibaijuka imekuja siku moja baada ya kambi ya upinzani bungeni kupitia Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee kutaja orodha ndefu ya vigogo hao wa CCM wakiwamo Marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Mawaziri Wakuu wastaafu, John Malecela na Frederick Sumaye.

Wengine waliotajwa ni Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Philip Mangula na aliyekuwa Naibu wake (Bara), Hassan Ngwilizi akisema kwamba wamehodhi ardhi kubwa mkoani Morogoro bila kuiendeleza. Hata hivyo, alisema ni