Monday, May 23, 2011

Ferguson aonywa na FA dhidi ya mwamuzi

Sir Alex Ferguson
Sir Alex Ferguson
Tume ya mienendo ya Chama cha England-FA, imemuonya Sir Alex Ferguson kuhusiana na matamshi yake siku zijazo baada ya matamsi yake dhdi ya mwamuzi Howard Webb. 
Matamshi hayo
yalitolewa na meneja huyo wa Manchester United kabla ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Chelsea, ambapo Manchester United ilishinda mabao 2-1 tarehe 8 mwezi wa Mei.
Licha ya Ferguson kumzungumzia Webb, amevunja taratibu za FA ambapo meneja yeyote hatakiwi kumzungumzia mwamuzi kabla ya mchezo.
"Alivunja taratibu kwa kiasi kidogo, lakini hata hivyo alikiuka taratibu," taarifa ya FA iliongeza.
Mwenyekiti wa tume hiyo alisema: "Taratibu za uamuzi huu ziliwekwa mwanzoni mwa msimu wa 2009/10 na ukarudiwa tena rasmi kwa vilabu tarehe 21 mwezi wa Oktoba 2010.
"Huku ni kwenda kinyume na taratibu zilizowekwa na ni mara ya kwanza hoja hiyo kusikilizwa na tume.
"Matokeo yake kuhusiana na mashtaka haya, tume ilikuwa ikifahamu juu ya matukio mengine ambapo matamshi kabla ya mechi yalitolewa na mameneja wengine.
"Katika shauri hili, ilichukuliwa kama ni kuvunjwa kwa taratibu kwa kiasi kidogo na onyo litolewe kwa mameneja wote kwa siku zijazo kwamba wakienda kinyume na taratibu, hata wakitoa matamshi ya mazuri ambayo pengine yataharibu amani, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao."
Siku mbili kabla ya mchezo baina ya Manchester United dhidi ya Chelsea - ambapo Chelsea wangeshinda wangeongoza msimamo wa ligi - Ferguson katika mkutano na waandishi wa habari alimzungumzia Webb.
Wakati huo alisema: "Tumempata mwamuzi mzuri, hakuna shaka yoyote kuhusiana na hilo."
"Lakini wasiwasi wetu mkubwa ni kupata matokeo mabaya."
"Tunao wachezaji wazuri wa kufanya vizuri. Tunatumai ni wakati wetu kupata angalao bahati kidogo."
Ni hivi karibu Ferguson alimaliza adhabu yake ya kufungiwa kukaa katika benchi la ufundi la timu yake kwa michezo mitano na pia alipigwa faini ya paundi 30,000kutokana na kumshutumu mwamuzi Martin Atkinson baada ya kufungwa mabao 2-1 na Chelsea mwezi wa Machi.

No comments:

Post a Comment