Kwa mujibu wa kiongozi mmoja mwandamizi wa soka kutoka Ghana, hakuna uhakika wa Sepp Blatter kama atapata kila kura ya Afrika katika uchaguzi wa Fifa utakaofanyika wiki ijayo.Fred Papoe, Makamu wa
Rais wa Chama cha Soka cha Ghana (GFA), amekiri "kuna uwezekano" baadhi ya nchi huenda zikamnyima kura Blatter.Siku ya Jumamosi, Papoe alikuwa mmoja wa wawakilishi 37 wa Afrika kumuidhinisha Blatter akiwa anachuana vikali na Mohammed Bin Hamman wa Qatar.
Tamko la siku ya Jumamosi la kumuunga mkono lililotolewa mjini Johannesburg linafuatia taarifa kutoka Caf ya mapema mwezi huu.
Lakini Papoe ameiambia BBC kwamba hakuna uhakika wa moja kwa moja kila nchi kama itafuata yaliyoandikwa.
Amesema: "Ulikuwa ni uamuzi wa pamoja uliochukuliwa na wote waliohudhria, lakini pia unaweza kugundua tulijiweka kando kuweka saini za tamko hilo.
"Wajumbe walihemewa na kumuunga mkono Bw Blatter - amefanya vizuri sana na hakuna haja ya kubadilisha timu inayoshinda.
"Lakini tunazungumzia kuhusu uchaguzi unaofanyika kwa siri, kwa hiyo hakuna uhakika."
Blatter anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi kwa mara muhula wa nne wakati wa uchaguzi wa Rais wa Fifa utakaofanyika tarehe 1 mwezi wa Juni mjini Zurich.
No comments:
Post a Comment