Monday, May 23, 2011

Uganda waonywa kuhusu kupiga honi

Dr Kiiza Besigye
Polisi nchini Uganda imewaonya watu waliopanga kupiga honi za magari kwa nia ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha watakamatwa kwa madai ya kuchafua mazingira kwa njia ya makelele.
Wito wa upinzani wa kupiga honi au kupiga miluzi mitano saa 11 jioni Afrika Mashariki ni kukamilisha maandamano ya "kutembea kazini" yalianza mwezi Aprili.
Makundi ya kutetea haki za
binadamu yamekosoa hatua kali zinazofanywa na polisi dhidi ya waandamanaji ambapo watu tisa walifariki dunia.
Mwezi huu Bw Yoweri Museveni aliapishwa kwa mara ya nne kuwa rais.
Alisema anataka sheria mpya ya kumnyima mtu dhamana kwa miezi sita kwa wale watakaokamatwa wakihusishwa kufanya ghasia au kusababisha uharibifu wa kiuchumi.
Kiongozi mkuu wa upinzani Kizza Besigye alikamatwa mara nne na kuwekwa chini ya kifungo cha udhibiti mara moja tangu maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha na mafuta kupanda.
Serikali inamshutumu kwa kujaribu kuandaa ghasia kama za Misri baada ya kushindwa kwenye uchaguzi.
Waziri wa Uingereza wa masuala ya Afrika, Henry Bellingham, alisema "mbinu nzito sana" zinazotumiwa dhidi ya Dr Besigye zinaipa wasiwasi serikali ya Uingereza, mmoja wa wafadhili wakubwa wa Uganda.

No comments:

Post a Comment