Takriban watu 11 wameuawa na wanamgambo katika shambulizi la mabomu na bunduki lililolenga katika kambi ya jeshi mjini Karachi, Pakistan.
Mmoja wa waliouawa ni afisa wa kijeshi mwenye uraia wa kigeni.
Maafisa wamesema zaidi ya wanamgambo kumi walihusika kwenye
shambulio hilo.Shambulio hili ni la tatu kulenga kambi hiyo tangu Aprili 26.
Kundi la Taleban tawi la Pakistan limekiri kuhusika na mashambulio ya hapo awali.
Miale ya moto imekuwa ikionekana kwa umbali huku milio ya risasi ikisikika kati ya wanajeshi na wanamgambo walioingia kambini hiyo.
Maafisa wa usalama wameambia BBC kwamba wanamgambo kadhaa walivamia kambi ya jeshi yenye ulinzi mkali kati kati mwa Karachi.
Walioshuhudia wamesema wanamgambo walitumia makombora kuharibu ndege za kivita zinazomilikiwa na jeshi la Pakistan.
Baadaye wanamgambo walianza kufyatua risasi hewani kiholela na kuwaua maafisa kadhaa wa kijeshi.
Katika kujibu mashambulio majeshi yalijaribu kuwafyatuliwa risasi wanamgambo hao.
Kufikia sasa majeshi zaidi yametumwa katika kituo hicho ambapo yameweza kuingia na kukabiliana na wapiganaji.
Baadhi ya wanamgambo wamewateka maafisa wa kijeshi ndani ya majengo ya kambi hiyo.
Shambulio la kambi ya Mehran ndilo la karibuni kufuatia mauaji ya kiongozi wa mtandao wa Al Qaeda Osama Bin Laden.
No comments:
Post a Comment