Monday, May 23, 2011

VIBONDE WA SIMBA SC WASHUKA DARAJA ENGLAND

Birmingham imeteremka daraja na msimu ujao itacheza ligi daraja la kwanza maarufu Championship, baada ya Roman Pavlyuchenko kufunga bao la pili dakika ya mwisho ya mchezo na kuipatia Tottenham, nafasi ya tano.
Ligi Kuu ya Soka ya England msimu wa 2010/2011 yamalizika
Ligi Kuu ya Soka ya England msimu wa 2010/2011 yamalizika
Wakati hali ya mambo ilipoonekana kuwaendea vizuri, Birmingham walionekana kuwa katika hali salama baada ya Craig Gardner kusawazisha bao la kwanza la Tottenham lililofungwa pia na Pavlyuchenko.
Lakini bao la pili la Wolves katika mechi yao dhidi ya Blackburn walipofungwa 3-2 nyumbani kwao, liliisukuma Birmingham katika
timu tatu za mwisho za kushuka daraja.
Na bao la pili la Pavlyuchenko katika dakika ya mwisho ya mchezo liliihakikishia Birmingham kuteremka daraja msimu huu.
Nao Blackpool wamemaliza ligi ya msimu huu kwa hali ya unyonge baada ya kufungwa mabao 4-2 na mabingwa Manchester United, hali iliyowafanya nao waungane na Birmingham pamoja na West Ham kushuka daraja katika ligi kuu ya soka ya England msimu huu.
Park Ji-sung aliipatia bao la kuongoza Manchester United kabla ya mkwaju wa free-kick uliopigwa na Charlie Adam kuipatia Blackpool bao la kusawazisha.
Gary Taylor-Fletcher aliweza kuipatia Blackpool bao la pili na ubao wa mabao ukasomeka 2-1 kabla ya Anderson kusawazisha na kufanya matokeo 2-2.
Ian Evatt alijifunga mwenyewe na kuipatia Manchester United bao la tatu na Michael Owen akamalizia kazi kwa kufunga bao la nne lililozidi kuizamisha katika nafasi ya kushuka daraja Blackpool.
Baada ya mchezo huo Manchester United walikabidhiwa kombe lao la ubingwa wa Ligi ya England kwa msimu wa 2010/2011.
Ferguson akishangilia baada ya mchezo
Ferguson akishangilia baada ya mchezo
Nao mabingwa wa msimu uliopita Chelsea walimaliza ligi kwa kufungwa bao 1-0 na Everton, bao lililofungwa na Jermaine Beckford. Katika mchezo huo Everton walicheza wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja baada ya Seamus Coleman kuoneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu John Obi Mikel.
Manchester City wamekamilisha msimu wa ligi kwa kushika nafasi ya tau baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bolton na moja kwa moja watacheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu ujao ikiwa ni nafasi ya juu kumaliza tangu mwaka 1977.
Baada ya kupoteza nafasi nyingi za kufunga hatimaye Joleon Lescott alifunga bao la kwanza kwa kichwa muda mfupi kabla ya mapumziko.
Bolton walijitahidi kupigana kiume kusawazisha lakini hali haikuwa njema upande wao kwani katika dakika ya 62 Edin Dzeko alifunga bao la pili.
Na bao la kusawaisha lililofungwa na Theo Walcott dakika za mwisho za mchezo, liliiwezesha Arsenal kutoka sare ya mabao 2-2 na Fulham na kuiokoa timu hiyo isiadhiriwe katika mchezo wa kufunga dimba.
Walcot aliyeingia kipindi cha pili alifanya juhudi binafsi za kupiga chenga na kukimbia na mpira kabla ya kuachia mkwaju uliojaa wavuni na kuisawazishia timu yake iliyokuwa imeshalala mabao 2-1 dhidi ya Fulham waliokuwa wakicheza kumi baada ya Zoltan Gera kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu mbaya Thomas Vermaelean.
Steve Sidwell ndiye aliiyeipatia bao la kwanza Fulham baada ya kazi nzuri ya Bobby Zamora ya kuchonga majaro ya pembeni kabla Robin van Persie kusawazisha.
Zamora aliifungia Fulham bao la pili kwa kichwa na kuifanya Fulham iongoze kwa mabao 2-1 to Fulham, kabla ya Walcott kusawazisha zikiwa zimesalia dakika chache kabla mchezo haujamalizika.
Matokeo hayo maana yake timu hizo mbili hazikumaliza msimu wa ligi kama zilivyokuwa zikitarajia - Arsenal ilikuwa na matumaini ya kumaliza nafasi ya tatu hali ingewawezesha kucheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya moja kwa moja, wakati Fulham walikuwa na lengo la kumaliza katika timu nafasi ya saba hali iliyowafanya wamalize nafasi ya nane.
Matokeo mengine ya mechi za kumalizia msimu wa Ligi msimu wa 2010/2011 ni kama jedwali linavyoonesha.

No comments:

Post a Comment