Sunday, June 5, 2011

Ivory Coast yaichapa Benin 6-2, taifa stars yatandikwa 2-1 na jamhuri ya kati,.... pata matokeo mengine kwa mechi zote zilizochezwa hiyo jana pamoja na vinara wa makundi.

kombe la mataifa ya Afrika
Michuano ya soka ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika yamefanyika. Katika joto hilo Kocha wa Algeria - Abdelhak Benchikha amejiuzulu mapema leo baada ya kuchukizwa na kipigo Timu yake ilichopewa na watani wake Morocco 4-0.

Mabao ya Morocco yalipatikana kupitia Mehdi Benatia na mshambuliaji wa Arsenal Marouane Chamakh katika kipindi cha kwanza na katika kipindi cha pili mji wa Marrakech ulilipuka kwa vifijo kufuatia mabao ya Youssouf Hadji na Oussama Assaidi yaliyopatikana dakika tisa baada ya kipenga cha kuanza kipindi cha pili.
Hivyo Morocco ikalipiza kisasi cha bao moja ililofungwa katika duru ya kwanza miezi mitatu iliyopita. Morocco ina pointi saba huku Jamhuri ya kati, Tanzania na Algeria zote zina pointi nne kila moja.
kufuzu mwaka 2012
Wawakilishi wengine wa Afrika kwenye kombe la Dunia mwaka jana Cameroon walijikuta nyuma ya Senegal kwa pointi tano baada ya kutoka sare ya 0-0 nyumbani mjini Yaounde hapo jana.
Ilibidi Polisi watumie gesi ya
kutoza machozi kuwatawanya mashabiki wa nyumbani waliolizingira gari la Timu ya Senegal kwenye uwanja wa Ahmadou Ahidjo.
Mshambuliaji Samuel Eto'o alishindwa kufunga bao la peneti akigonga mwamba dakika za majeruhi. Kibarua kwa Cameroon ni kuzifunga Mauritius na Jamhuri ya Congo katika mechi zilizosalia ili kurejesha matumaini ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa mara ya tisa mfululizo.
Ghana kwa upande wake imezidi kuimarisha matumaini yake kwa kuibwaga Congo Brazaville 3-1 mjini Kumasi.
Ghana ilipata magoli yake katika kipindi cha pili kupitia Isaac Vorsah, Prince Tagoe na Emmanuel Agyemang-Badu. Bao la Congo likapatikana Matt Moussilou.
Kwa ushindi huo Ghana inaongoza kundi la 1 ikiwa na pointi 10 ikifuatiwa na Sudan inayocheza leo na Swaziland ikiwa na pointi saba. Congo ambayo ni ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi tatu haiwezi tena kufuzu.
Matumaini ya mashabiki wa Zambia yalizidi kuimarika baada ya Chipolopolo kuizaba Msumbiji matatu kwa sufuri katika kundi C mjini Lusaka hapo jana.
Chris Katongo alifunga mabao mawili na Collins Mbesuma kumalizia kwa bao la tatu.
Kwa ushindi huo Zambia sasa inaongoza kundi C kwa pointi 9 mbili zaidi ya Libya inayochuana na Comoro leo.
Matumaini ya Msumbiji yametoweka baada ya mechi hii wakiwa na pointi tatu kutoka mechi nne halikadhalika Comoro nao tayari hawatoshiriki wakiwa nyuma ya Msumbiji kwa pointi.
Comoro ilikuwa nyumbani kuipokea Libya na matokeo yake ni Comoro 1 Libya 1
Tanzania ilikuwa ugenini Jamhuri ya Afrika ya kati. Licha ya bao la Mbwana Samata aliyeletwa baadaye na kusawazisha.
Jamhuri ya kati ikapata bao lake la ushindi dakika tatu kabla ya kipenga cha mwisho na hivyo kujiweka nafasi ya pili ya katika kundi nyuma ya Morocco kwa tofauti ya magoli.
Tanzania ni ya tatu kwa tofauti ya magoli na Algeria inayoburura mkia. Juhudi za Tanzania ziliwatia homa mashabiki wa timu ya nyumbani lakini washambuliaji kama Athuman Machupa walipoteza fursa nyingi kuivusha Taifa Stars.
Kenya iliyotazamiwa kuwika mjini Luanda, Angola ilipoteza mechi yake dhidi ya Angola. Mechi ikimalizika 1-0.Matokeo hayo yanaipandisha Angola hadi nafasi ya pili kwa pointi 6 nyuma ya Uganda yenye pointi 10.
Uganda ilipiga hatua kwa kuichapa Guinnea Bissau 2-0 mjini Kampala. Hivyo Uganda inaongoza kundi la K ikiwa na pointi 10.
Baada ya ushindi huo Uganda Cranes, ikifunzwa na Kocha kutoka Scotland Bobby Williamson, ina safari ya Luanda kuchuana na Angola kabla ya mchi yake ya mwisho dhidi ya mahasimu wake wakuu Harambee stars nchini Kenya.
Burkina Faso ilikaribia kufuzu kwa ushindi wake mkubwa wa 4-1 dhidi ya Namibia mjini Windhoek.
Abdul Razak Traore alifungua mtiririko wa magoli mnamo dakika ya 12 yakifuatiwa na mikwaju miwili ya peneti iliyotiwa kimyani na washambuliaji Aristide Bance na la tatu likafungwa na Alain Traore katika kundi F.
Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo iliichapa Mauritius nyumbani kwao 2-1 licha ya wenyeji kuliona lango mapema katika kipindi cha kwanza.
Nigeria ikicheza ugenini mjini Addis Ababa ilitarajia kupata vibonde lakini licha ya kutangulia Ethiopia ikarudisha na kufikia mapumziko ikawa ni 1-1 kipindi cha pili Nigeria ikitumia kila ujanja ilipata bao la kuongoza lakini Ethiopia ikakataa kuonewa nyumbani kwa kurudisha bao hilo na hadi kipenga chja mwisho Ethiopia 2 Nigeria 2.
Zimbabwe ikicheza nyumbani ilianza vyema kwa kuliona lango na kufunga bao mapema lakini Mali ikarudisha bao kupitia El Hadji Mohammad Traore hadi dakika za mwisho Zimbabwe ilipozidisha kasi na kupata bao lake la ushindi kupitia Knowledge Musona kupitia mkwaju wa peneti.
Nchini Botswana, Malawi ililazimisha sare ya kutofungana na Timu ya nchi hiyo ambayo imeisha fuzu kwa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon na Equatorial Guinea.
Burundi ikicheza nyumbani ikairarua Rwanda 3-1 kwa mabao yaliyotiwa kimyani na Seremani Ndikumana aliyefunga bao katika kipinmdi cha kwanza. Hadi mapumziko Burundi ikaongoza 1-0 dhidi ya Rwanda.
Habari hizi bila shaka ziliwafurahisha mashabiki wa Ivory Coast iliyokuwa uwanjani kuchuana na Benin. Hata hivyo Ivory Coast haikuhitaji kusaidiwa kazi hiyo ikifumania nyavu za Benin mara tatu.
Hata hivyo mpira unadunda na Benin ilitafuta nguvu za ziada na kurudisha angalau mabao mawili. Kujibu nguvu hiyo wachezaji wa Ivory Coast walizidisha malumbano na kumaliza udhia kwa kuikandika Benin 6-2.
Baadhi ya matokeo ni kundi makundi ni kama ifuatavyo:
Group E: Mauritius 1-2 DR Congo.
Group C: Comoros 1-1 Libya.
Group K: Botswana 0-0 Malawi.
Group A: Zimbabwe 2-1 Mali.
Group B: Ethiopia 2-2 Nigeria.
Group H: Benin 2-6 Ivory Coast.
Group I: Swaziland 1-2 Sudan.
Group H: Burundi 3-1 Rwanda.
Group D: Afrika ya Kati 2-1 Tanzania.
Group J: Angola 1-0 Kenya.
Group A: Liberia 1-0 Cape Verde.
Group K:Tunisia 2-0 Chad
Mechi kali ambayo inatarajiwa ni kutoka kundi G mjini Cairo ambako Timu iliyoshinda Kombe la Mataifa ya Afrika mara nyingi kuliko nyingine Misri ina kibarua leo cha uwezekano mkubwa wa kukosa kufuzu endapo itapoteza dhidi ya Bafanabafana.
Pamoja na mechi hiyo bado tunasubiri matokeo ya mechi za kundi B: Guinea ikichuana na Madagascar
na kutoka kundi K: Tunisia na Chad.

No comments:

Post a Comment