Sunday, June 5, 2011

Libya inashambulia helikopta za NATO

Helikopta za Uingereza zilizotumika kwa mara ya kwanza kurusha makombora dhidi ya sehemu za Libya zimeshambuliwa na jeshi la Kanali Gaddafi.
Mashua wanawaondoa wakimbizi kutoka lIbya
Mwandishi wa BBC kwenye manuwari ya jeshi la wanamaji la Uingereza, Royal Navy, katika pwani ya Libya, anasema helikopta mbili za aina ya Apache katika manuwari hiyo, zilishambulia kituo cha radar na kituo cha ukaguzi cha
jeshi, karibu na mji wa Brega.
Helikopta hizo zilirudi kwenye manuwari salama na rubani mmoja alisema ametosheka na matokeo:
"Tumefurahi namna operesheni ilivotekelezwa.
Hizi helikopta zimeundwa hivo, zinakutumikia sawa-sawa na kukurudisha ardhini salama".
Helikopta za Ufaransa zilishiriki katika operesheni hiyo na kuzilenga shabaha nyengine.
NATO inasema inatumia helikopta kufanya mashambulizi, ili kuweza kuzuwia jeshi la serikali ya Libya kuwalenga raia wanaopigana nalo

No comments:

Post a Comment