MH. Rozi Wilbard, mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke baada ya kuahirishwa kwa mkutano huo.
Mwanaharakati anayechipukia VENANACE MREMA(supersonic) akiwa na mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Temeke mh. ROZI WILBARD baada ya mkutano huo kuahirishwa.
Mmoja wa makada wa chama aliyehudhuria mkutano huo, akishushwa jukwaani mara baada ya kupatwa na mshtuko wakati wa maandalizi ya mkutano huo hapo leo.
Askari wa kituo cha polisi cha KIGAMBONI akiwasili uwanjani hapo mara tu baada ya mkutano huo kuahirishwa, kama kawaida kila inapokuwepo mkutano wa CHADEMA mambo kama hayo huwa hayakosekani.
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Temeke bi Rozi Wilbard akilizungumzia kwa machungu swala la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa chama cha Chadema MH. FREEMAN MBOWE.
Mwanaharakati anayekuja juu kwa kasi VENANCE MREMA(supersonic), akiwa na mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Temeke Bi.ROZI WILBARD mara baada ya kuahirishwa kwa mkutano huo.
wanaharakati mashuhuri nao hawakuwa nyuma katika kuzielezea hisia zao katika mkutano huo.
Baadhi ya wakereketwa wa demokrasia waliohudhuria katika mkutano huo.
Mmoja wa makada wa CHADEMA aliyepata stress kabla ya kuanza kwa mkutano huo hapo leo.
Akizungumza na wananchi waliofika katika viwanja hivyo mwenyekiti wa chama hicho katika wilaya ya temeke mh. Rozi Wilbard amesema waheshimiwa wabunge hao akiwemo mh.Wenje na Joseph Mbilinyi walishindwa kuwepo kutokana na kuwepo katika kikao na kamati kuu ya chama ili kujadiliana juu ya kukamatwa mwenyekitiwa chama hicho mheshimiwa Freeman Mbowe. mh. Mbowe alikamatwa jana jioni baada ya amri kutoka kwa mahakama kwa madai kuwa alifanya mikutano ya hadhara bila kibali kinyume cha sheria na pia kudaiwa kuchochea maandamano.Aidha bi Rozi hakutanabaisha ni linimkutano huo utatangazwa tena.
No comments:
Post a Comment