Monday, May 30, 2011

Mlipuko wa bomu waua 10 Nigeria

Goodluck Jonathan


Nigeria
Nigeria

Karibu watu 10 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa baada ya bomu kulipuka karibu na kambi ya jeshi Kaskazini mwa Nigeria,maafisa katika eneo hilo wamesema.
Mlipuko huo ulitokea katika soko la Mamy mjini Bauchi siku ya Jumapili.
Watu waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.
Kufikia sasa hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika na shambulio hilo.
Shambulio limetokea saa chache baada ya Goodluck Jonathan kuapishwa kwa muhula mpya wa miaka minne kama rais katika mji mkuu wa
Nigeria, Abuja.
Mlipuko mwingine ulitokea katika klabu cha pombe viungani mwa mji wa Abuja na kusababisha majeraha madogo, maafisa wanasema.
Goodluck Jonathan
Sababu ya mlipuko huo haikuweza kufahamika mara moja.
Taarifa zingine zinasema kuwa kumekuwepo na milipuko mitatu katika muda mchache.
"kulikuwa na watu wengi kwa kuwa ni Jumapili jioni. Watu walikuwa wanaburudika,wanakula na kunywa," Kamishna wa polisi wa jimbo la Bauchi Abdulkadir Indabawa alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema.
Kambi za jeshi nchini Nigeria mara nyingine zinakuwa na sehemu ya soko ambako wafanyabiashara wanauza vyakula,vinywaji na bidhaa zengine kwa wanajeshi na raia.
Barabara za kuelekea kwenye kambi za kijeshi zilifungwa na maafisa wa usalama.

No comments:

Post a Comment