Matumaini ya mashabiki wa Manchester United pamoja na wakuu wa chama cha mpira England yalikuwa makubwa kwa Sir Alex Ferguson kutwaa kombe la pili katika msimu mmoja baada ya kushinda Ligi ya England na licha ya kushindwa kutwaa kombe la FA na la Carling.
Fainali ya mwaka huu ikichezwa kwenye uwanja wa Wembley ilionekana kuwapendelea Manchester United ambao katika michuano yote ya kufuzu kufikia hapa hawakupoteza mechi hata moja.
Mchuano ulianza kwa vijana wa Man.united kuonyesha uwezo wa kuikaba Barcelona koo.
Hali hiyo iliendelea kwa dakika kumi za kipindi cha kwanza na mnamo dakika ya 27 Pedrito akapenya lango la Man.United
Licha ya Barca kutangulia kwa bao la Pedrito Man.united wakatumia makosa ya Barca kusinzia na Wayne Rooney kupachika bao ambalo baadhi ya wadadisi walidhani lilitokana na kosa baada ya mchezaji wa Barca kusukumwa na mpira wa Rooney kumpata Ryan Giggs katika hali ya
kuotea.Hadi mapumziko hali ilikuwa ni moja Barcelona na moja Man.united.
Kipindi cha pili kama alivyoshauri Sir Alex Ferguson vijana wake wakarudi na hamu tofauti na kuanza kwa kasi lakini Lionel Messi aliyegeuka mwiba kwa mabeki wa Man.United akatoa kombora kutoka umbali wa mita 25.
Tangu hapa vijana wa Man.United walizungushwa kuutafuta mpira lakini vijana wa Barca waliudhibiti vilivyo na punde si punde David Villa ambaye makombora yake kabla ya hapo yalipetwa na goalkeeper Van De Sar aliupata mpira kutokana na makosa ya Nani na kuusukuma kimyani kutikisa nyavu za Man.Utd kwa mara ya tatu jana.
Mmoja wa viongozi wa soka nchini Uingereza akiwa ni Kocha mwenye sifa ya kuichezea Timu ya England Graham Taylor alisema kuwa Manchester United hawajazowea kuchezewa mpira wa pasi za aina hiii na ni mara ya pili wanashindwa kukabiliana na klabu inayodhibiti mpira na nitasema kwamba kama kuna sababu ya kusikitikia ni kwamba hapana sababu yoyote ya kuwatetea bali ukweli ni kwamba wachezaji wameonekana kama wasiojua wafanye nini, wameduaa uwanjani bila kujua la kufanya.
Yeye kocha wa Man.United Sir Alex Ferguson alikiri moja kwa moja kwamba Barcelona ndiyo Timu kali aliyowahi kukabiliana nayo katika fainali ya Ligi ya mabingwa.
Klabu hiyo ya Uhispania ilitoa funzo uwanjani kwa pasi zao za kuvutia na kumalizia vizuri kujishindia Kombe la Ulaya kwa mara ya nne.
Alimsifu mchezaji mmoja Lionel Messi akisema kuwa Mabeki wake walishindwa kumkaba na si kosa lao ni kijana asiyeshikika.
Kocha wa Barcelona pia alimimina sifa zake kwa mchezaji huyo na kusema bila Messi Barcelona hukosa chachu, hukosa muelekeo.
Na kufuatia matokeo hayo ya ushindi wa Kombe la Ulaya na kukusanya jumla ya magoli 53 katika msimu mmoja linalomsubiri Messi kwa sasa ni zawadi ya mchezaji bora wa FIFA kwa mara ya tatu.
Akiwa mwenye umri mdogo wa miaka 23 ana mda mrefu mbele yake kushinda tuzo nyingi.
Bao lake moja katika fainali ya Wembley huenda haitoshi kuelezea mchango wake kwa ujumla.
Ni Messi aliyetafuta mianya kupasua ngome ya Man.United kuwapasia wenzake mipira kutafuta ushindi na kuifanya klabu nzima ya Man.united ionekane kama watoto wa shule wanaojaribu kuiga mchezo wa wachezaji wenye uzowefu.
No comments:
Post a Comment