Monday, May 30, 2011

Bin Hammam kutowania madaraka FIFA

Mohamed Bin Hammam kutoka Qatar, ameelezea kwamba amejiondoa katika uchaguzi wa kuwania madaraka ya rais wa shirikisho la kimataifa la soka, FIFA.
Mohamed Bin Hammam
Mohamed Bin Hammam
Bin Hammam, mwenye umri wa miaka 62, alitangaza hatua hiyo saa chache kabla ya kufika mbele ya tume ya maadili kujibu madai ya kuhusika katika kupokea mlungula.
Mkuu huyo wa mashirikisho ya soka ya bara Asia, alisema nia yake ni kuliepusha jina la shirikisho la FIFA kuharibiwa sifa kwa kupakwa matope.
Bin Hammam alikuwa anatazamiwa kupambana na rais wa shirikisho hilo, Sepp Blatter, ambaye pia anachungwa na kamati hiyo ya maadili.
Wote wawili wanakanusha lawama za kupokea hongo

No comments:

Post a Comment