Rais wa shirikisho la kimataifa la soka, FIFA, Sepp Blatter, itabidi kujitokeza mbele ya kamati ya shirikisho hilo inayohusika na maadili, ikiwa ni hatua ya uchunguzi wa madai kwamba maafisa wa juu wa shirikisho hilo kupokea hongo.
Blatter ameitwa na kamati hiyo pamoja na maafisa wenzake wa bodi, Jack Warner na Mohammed Bin Hammam.
Kamati hiyo itawasikiliza keshokutwa Jumapili.
Blatter ameamriwa kufika mbele ya kamati hiyo, baada ya
mpinzani wake katika kuwania kiti cha urais wa FIFA, Mohamed Bin Hammam kusema kwamba Blatter anafahamu juu ya madai hayo ya kupokea mlungula katika shirikisho hilo.Hayo yakiendelea, waziri wa michezo na olimpiki wa Uingereza, Hugh Robertson, amelitaka shirikisho la soka la FIFA kuahirisha uchaguzi wa rais wa shirikisho hilo, hadi uchunguzi wa madai hayo ya ufisadi kukamilika.
Bw Robertson amesema kutokana na madai hayo ya ufisadi, ni vigumu kwa watu kuweza kupiga kura kikamilifu
No comments:
Post a Comment