Monday, May 30, 2011

Ujerumani kuvimaliza vinu vya nuklia

Kufuatia mazungumzo ya usiku kutwa ya serikali ya mseto nchini Ujerumani, nchi hiyo imetangaza kubadilisha sera kuhusiana na nguvu za nuklia.
Mjerumani katika maandamano
Mtu aliyebeba bango ambalo linauliza; 'Nguvu za nuklia? - La, hasha!'
Ujerumani imetangaza kwamba itakomesha utumizi wa vinu 17 vya nguvu za nuklia kufikia mwaka 2022.
Uamuzi huo unaifanya Ujerumani kuwa taifa la kwanza kubwa ambalo limeendelea sana kiviwanda kutangaza kutupilia mbali utumizi wa nguvu za nuklia.
Mataifa kadhaa yamekuwa yakizichunguza sera zake kuhusiana na nguvu za nuklia, hasa kufuatia janga la Fukushima nchini Japan, mwezi Machi.
Nchi ya Uswisi wiki iliyopita ilikuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kutangaza kwamba itasimamisha utumizi wa
nguvu za nuklia

No comments:

Post a Comment