Wednesday, August 24, 2011

Welbeck ang'ara United .

venance.chadema@yahoo.com

 
Tuesday, 23 August 2011 20:54


MSHAMBULIAJI Danny Welbeck alifunga bao moja na kutengeneza pasi ya bao lingine wakati Manchester United ilipoichapa mabao 3-0 Tottenham Hotspur katika mechi ya Ligi Kuu England iliyofanyika juzi kwenye uwanja wa Old Trafford.

Katika mechi hiyo kocha wa Manchester United, Alex Ferguson aliamua kupanga wachezaji vijana ambapo vijana hao hawakumuangusha kwani Welbeck alifunga bao la kwanza baada ya kuunganisha vizuri kwa kichwa krosi ya kijana mwenzake Tom Cleverley.

Katika dakika ya 76, Welbeck alitoa pasi nzuri ya kisigino akiwa ndani ya sita ambayo ilimkuta Anderson aliyeandika bao la tatu na bao la tatu lilifungwa na Wayne Rooney.

"Katika kipindi cha pili tulitawala, hiyo inaonyesha United tunapenda wachezaji vijana kwa sababu nilikuwa nimepanga vijana na mmeona uwezo waliokuwa nao, uwezo waliouonyesha katika kipindi cha pili ni uwezo wa aina yake, pia walicheza mechi ya kasi mwanzo mpaka mwisho,"alisema Ferguson.

Pia katika mechi hiyo winga mahiri wa Manchester United, Ashley Young alicheza vizuri sana na kuisumbua ngome ya Tottenham.

"Kocha alitupatia maneno ya busara wakati wa mapumziko ambapo alituambia tujitume zaidi, pia alitueleza kila pointi katika ligi ni muhimu hivyo tunatakiwa tushinde kadri tunavyoweza,"alisema Welbeck ambaye alikuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.

Naye kocha wa Tottenham, Redknapp alisema,"Manchester United walikuwa hawana chochote ila walipopata bao la kwanza bao hilo liliwabadilisha na kuwapa nguvu zaidi yetu."

No comments:

Post a Comment