venance.chadema@yahoo.com
Tuesday, 23 August 2011 20:12 |
WAFANYABIASHARA wa nguo na viatu wamelalamikiwa kwa kupandisha bei ya bidhaa, wakati wa kuelekea kwenye Sikukuu ya Iddi.Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam walisema bei ya nguo na viatu vya watoto imepanda, hali itakayosababisha wazazi wengi kushindwa kumudu.
“Hali imekuwa ngumu wakati huu, nguo zimepanda bei na hatuna uwezo, sijui watoto wetu watavaa nini sikukuu,” alilalamika mwanamke aliyetambulika kwa jina moja la Zubeda.
Wazazi wengi wakiwa na watoto walionekana kwenye maduka, wakifanya ununuzi wa nguo na viatu.
“Hawa wafanyabiashara wanafanya sikukuu ndiyo kipindi cha kuongeza mtaji na kupata faida kubwa, kitu ambacho siyo sahihi na kinatukandamiza wanyonge,” alisema Jamal Habibu
Baadhi ya wafanyabiashara walisema chanzo cha kupanda bei
hizo, ni kutokana na wanakochukua bidhaa hizo.
“Hatupandishi bei kwa ajili ya sikukuu kama watu wengi wanavyodhani, bali ni gharama za ununuzi tunakotoa bidhaa hizo,” alisema Kitwana Kassim, mmiliki wa duka la nguo eneo la Kariakoo.
Naye Erick Kishoka, mfanyabiashara wa viatu alikanusha kupanda kwa bei na kusisitiza kuwa, bado wanatumia zile za zamani bali wananchi hawanunui mara kwa mara. |
No comments:
Post a Comment