venance.chadema@yahoo.com
Tuesday, 23 August 2011 20:55 |
MSIMU mpya wa ligi ya Morocco umeanza kwa mabingwa watetezi Raja Casablanca kupoteza mchezo wao wa kwanza. Recreativo Libolo ilikalia kiti cha uongozi wa ligi ya Angola huku Red Arrows ikiendeleza rekodi yao ya kutofungwa Zambia. Nchini DR Congo, TP Mazembe Englebert imeendelea kupanda kileleni.
DR Congo Super League: Timu tatu kileleni
Kurejea kwa Tresor Mputu baada ya kifungo cha mwaka moja aliamsha hali mpya kwenye soka la Congo, mshambuliaji huyo alionyesha umuhimu wake kwenye kikosi cha Mazembe alipoiongoza kushinda 3-0 dhidi CS Don Bosco 3-0 jijini Lubumbashi. Matokeo hayo yameifanya Mazembe kufikisha pointi 19, moja nyuma ya vinara V Club
Mechi kubwa: Mputu alitangaza kumaliza kifungo chake kwa kuifungia goli Mazembe dhidi ya TS Malekesa wiki iliyopita, na mwishoni mwa wiki hii alitegeneza bao la kwanza kwa Mbwana Samata dakika ya 14 na kufunga la kwake dakika ya 20. Joel Kimuaki alihitimisha karamu hiyo ya mabao kwa kufunga la kwake kwa shuti kali la umbali dakika 68.
Zambia Super Division: Red Arrows imeendelea kupaa
Wakati msimu ukikaribia mwishoni vinara Red Arrows walilazimishwa sare 1-1 nyumbani na Roan United. Lakini bado wanaongoza kwa pointi tatu mbele ya Power Dynamos na Konkola Blades na pointi mbili zaidi kwa Zanaco inayoshika nafasi ya nne. Red Arrows, timu ya kikosi cha jeshi cha wanaanga, waliotwaa taji hilo kwa mara ya kwanza mwaka 2004.
Mechi kubwa: Power Dynamos iliiduwaza Konkola Blades kwa kushika nafasi ya pili baada ya kushinda 2-1 kwenye mchezo mkali uliofanyika mjini Kitwe. Felix Nyaende alifunga mabao yote mawili kwa Dynamos, ambao walifunga mechi mbili zilizopita.
Angola Girabola: Mbio za nane
Tofauti ya pointi nane zimezitenganisha timu nane za juu kwenye msimamo wa ligi yenye timu 16, kwa sasa zimebaki raundi nane msimu kumalizika. Libolo imeshikiria usukani kwa mara ya kwanza msimu huu, na kuwa mbele kwa pointi moja baada ya kulazimishwa sare na timu ya jeshi la Primeiro Agosto. Kabuscorp iliondolewa kwenye nafasi ya pili baada ya kufungwa 1-0 na mabingwa watetezi InterClube. Petro Atletico ilianguka nafasi ya tatu baada ya sare 2-2 na timu ya mkiani ya Benfica Luanda.
Mechi bora: Timu zote Primeiro Agosto na Recreativo Libolo walikuwa na nafasi ya kushikiria usukani wa Girabola, lakini sare matokeo ya sare yameifanya Libolo kuongoza ligi hiyo.
Morocco Botola: Kiza kinene
Mabingwa Raja Casablanca walifungwa kwenye msimu wao mpya kwa kipigo cha ugenini kutoka kwa KAC Kenitra kuendeleza rekodi yake mbovu iliyoanza katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Wawakilishi wengine wa Morocco kwenye michuano ya Afrika, Wydad Casablanca wamejiweka vizuri baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya IZ Khemisset.
Ligi nyingine
US Ouakam imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa kwanza wa ligi ya Senegal baada ya kuichapa Diaraf Dakar, huku Casa Sport inayoshika nafasi ya pili ikipokea kipigo.
Sunshine Stars ilichapa JUTH FC 2-0 kwenye mchezo muhimu uliowafanya sasa kuwa nyuma kwa pointi moja kwa vinara wa ligi ya Nigeria, Dolphin FC.
Vinara wa ligi ya Zimbabwe walikutana wiki hii mchezo uliowakutanisha FC Platinum dhidi Motor Action mechi iliyomalizika kwa sare. Timu zote zimefikisha pointi 41 katika mechi 21. |
No comments:
Post a Comment