Monday, June 6, 2011

Jaji awashangaa washukiwa Kenya

Mahakama

Mahakama ya Uingereza

Mahakama kuu ya Kenya imekataa ombi la mbunge mashuhuri nchini humo Chris Okemo na aliyekuwa mkurugenzi Mkuu wa shirika la umeme la kitaifa Samwel Gichuru la kiuzuia serikali kuwakamata na kuwapeleka Uingereza kujibu mashtaka ya ufisadi na uhalifu wa kiuchumi.
Jaji Nicholus Ombiji ameshangaa kwanini wawili hao wanababaika kwa kufika mahakamani wakati serikali ya Kenya yenyewe bado haijawasilisha kesi ya kuomba wakamatwe na kufikishwa katika mahakama ya visiwa vya Jersey nchini Uingereza.
Mahakama imemwambia Okemo ambaye wakati mmoja alikuwa waziri wa nishati na pia waziri wa fedha wa
Kenya pamoja na mwenzake kwamba hawana uwezo wa kumzuia mkuu wa sheria nchini humo kuagiza wafikishwe mbele ya mahakama ya Uingereza ili kujibu mashtaka ya ufisadi.
Mahakama ya Jesey imetoa agizo la kukamatwa kwa Okemo na Gichuru na kufikishwa mbele yake kutokana na madai ya kupokea mamilioni ya pesa kwa kutumia nyadhifa zao serikalini wakati huo na kuzificha katika taasisi mbali mbali za kifedha Uingereza.

No comments:

Post a Comment