Tuesday, June 7, 2011

Mbunge CUF, wenzake waachiwa kwa dhamana

 Send to a friend
Tuesday, 07 June 2011 20:54
Mustapha Kapalata,Tabora
HATIMAYE Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Magdalena Sakaya na wenzake 11 wameachiwa kwa dhamana.
Mbunge huyo na wenzake waliachiwa jana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Urambo, Oscar Bulugu, baada ya kutimiza masharti ya dhamana waliyopewa na mahakama hiyo, ingawa walipunguziwa masharti waliyopewa awali.

Masharti magumu yalikuwa ni kwa washtakiwa wanaotoka nje ya Wilaya ya Urambo, wakati wanaotoka ndani ya wilaya hiyo walitakiwa kuwa na barua ya mtendaji wa kata na walitimiza masharti ya kuwa na barua hizo.

Washtakiwa wote walishindwa kutimiza masharti waliyopewa na mahakama Jumatatu na kulazimika kurudishwa mahabusu, lakini upande wa utetezi uliomba masharti hayo kwa wanaotoka nje ya wilaya yapunguzwe na kuomba shauri hilo lisikizwe jana.

Baada ya kusikiliza kesi hiyo, mahakama ilikubali kupunguza masharti, huku wakipewa mengine ambayo walitimiza na kupewa dhamana hadi Juni 20, mwaka huu itakapotajwa tena kesi hiyo.

Waliopewa dhamana ambao wanatoka ndani ya wilaya, ni Msafiri Kaidi, Mkiwa Juma, Singu Yusto, Mrisho Sued, Chagu Salum, Zainab Said na  Peter Charles, huku wanaotoka nje ya wilaya mbali ya Sakaya, ni Doyo Hassan, Kiyungi Amri, Hashim Bakari na Yasin Mrutwa.

Miongoni mwa masharti ya dhamana hiyo, washtakiwa hawatakiwi kufika eneo la Shella, kulikotokea machafuko kati ya wananchi na polisi

No comments:

Post a Comment