SIKILIZA HABARI HIYO
Media Player
Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter amechaguliwa na wajumbe kuliongoza shirikisho hilo kwa muhula mwingine wa nne.
Uchaguzi huo unafuatia mtikisiko mkubwa katika shirikisho la FIFA , uliosababishwa na kashfa za rushwa zilizojitokeza siku kadhaa zilizopita na
kulazimisha baadhi ya maafisa kusimamishwa.Bwana Blatter mwenyewe pia alifikishwa mbele ya kamati ya maadili ya FIFA siku ya Jumapili kuchunguzwa kuhusiana na kashfa hizo hizo, lakini kamati ikaamua hana kesi ya kujibu.
Katika mjadala wa Dira ya Dunia
Je , imekuwa sahihi kuendelea na uchaguzi wa FIFA wakati shirikisho hilo likiandamwa na kashfa ?
Walishiriki katika mjadala huu ni
Israel Saria, Mchambuzi wetu wa maswala ya soka
Said El-maamry , mjumbe maalum katika kamati ya shirikisho la soka barani Afrika, na ameshiriki katika shughuli mbalimbali za Fifa
Juma Nkamia , ambaye mbali na kuwa mwandishi wa habari wa michezo ameshakuwa katika uongozi wa soka, na kwa sasa pia ni mbunge nchini Tanzania
Sam Nyamweya, Mwenyekiti wa KFF ambalo ni shirikisho la soka nchini KENYA
Rashid Alfred, mwandishi wa habari Burundi
No comments:
Post a Comment