Monday, June 6, 2011

Wanafunzi wataka serikali kusimamia bodi ya mikopo


Sunday, 05 June 2011 20:58
Happy Lazaro, Arusha
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Mount Meru, kimeomba serikali kuhakikisha inasimamia kikamilifu fedha za wanafunzi kupitia bodi ya mikopo.
Wakizungumza kwenye hafla ya kuchagua uongozi mpya wa serikali ya wanafunzi wa chuoni hapo, walisema fedha hizo zimekuwa hazina usimamizi mzuri na kuleta usumbufu kwao.

Rais anayemaliza muda yake, Ezekiel Meliary, alisema wanafunzi wengi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto lukuki, zinazotokana na bodi ya mikopo kutegemea fedha kutoka serikalini.

Meliary alisema asilimia 98 ya wanafunzi wanaosoma shahada ya elimu na elimu ya biashara, wanategemea zaidi mikopo kutoka serikalini , hivyo bodi ya mikopo imekuwa tatizo kubwa.

Alisema hali hiyo inasababisha kuwapo kwa migogoro wakati mwingine migomo isiyoisha kwenye vyuo
mbalimbali nchini.
“Wanaoteseka ni wanafunzi wenyewe, siyo chuo husika kwa sababu hakina mkataba na serikali, bali mwanafunzi ndiyo mwenye mkataba na serikali,” Meliary
.
Rais wa serikali ya wanafunzi aliyechaguliwa ni Janatu Selemani na Makamu wake, Benjamin Buromela.Seleman alisema changamoto kubwa ambayo wanaendelea kukabiliana nayo, ni kucheleweshwa kwa fedha za chakula na malazi, hali inayopelekea kuwaweka katika hali ngumu.

Alisema hali hiyo inaweza kusababisha wanafunzi kujiingiza katika mambo yasiyofaa kwa ajili ya kujikimu kwa maisha.
Naye Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Serikali ya Wanafunzi, Amani Laizer, alisema ili kuhakikisha wanafunzi hao wanakuwa na umoja, atajenga mawasiliano kati yao na vyuo vingine. 

No comments:

Post a Comment