Friday, June 3, 2011

Aina mpya ya Bakteria yazua mtafaruku

Shirika la Afya Duniani linasema kuwa kulipuka kwa maradhi yanayosababishwa na aina ya bakteria ajulikanaye kama E. coli nchini Ujerumani ni aina mpya kabisa ya bakteria.
Maambukizi yake yanaweza kusababisha hali hatari inayoathiri - mfumo wa damu na kibofu cha mkojo - haemolytic-uraemic syndrome - kwa kuathiri damu na maini.
Matango
onyo msitumie bila kuchemsha
Takriban watu 1,500 wamekumbwa na hali hii na wengine 17 wamefariki: 16 huko Ujerumani ma mmoja nchini Sweden.
Hapa Uingereza, raia watatu wameambukizwa kwa mujibu wa
Shirika linaloshughulikia masuala ya Afya.
Msemaji wa Shirika la Afya Duniani, Aphaluck Bhatiasevi,amenukuliwa akisema kuwa, mdudu huyu hajawahi kuonekana katika mlipuko wa aina yoyote Duniani.
Wataalamu kwenye Kituo cha Beijing kinachohusika na mifumo jeni huko Uchina nao wanasema kuwa huu ni mfumo mpya kabisa wa bakteria ambaye kasi yake ya maambukizo ni nyepesi yenye sumu.
Wachunguzi huko Ujerumani wanasema kuwa uchambuzi wao kuhusu bakteria huyu umedhihirisha aina mpya na ya kipekee ya bakeria.
Wanasema kuwa ana jeni mbili kutoka makundi mawili yanayofahamika ya E.Coli: enteroaggregative E. coli (EAEC) pamoja na enterohemorrhagic E. coli (EHEC).
Taasisi ya Afya ya hapa Uingereza ameiambia BBC kuwa ndiyo kwanza tunajifunza yanayoweza kujitokeza kuhusu mdudu huyu.
Ulaya
Mwanzoni ilidaiwa kuwa bakteria huyu alizuka kutoka matango kutoka Uhispania, ingawa madai hayo hayajabainika.
Mkuu wa Taasisi ijulikanayo kama Robert Koch, ambayo hufuatilia kwa karibu maambukizi ya aina yoyote huko Ujerumani, amesema kuwa kuzuka huku kwa maradhi haya huenda kukaendelea kwa miezi kadhaa na huenda tusijue chanzo chake.
Tayari kutokana na hali hiyo, Urusi imepiga marufuku mboga kutoka Muungano wa Ulaya na Mganga mkuu wa nchi hiyo ameonya kuwa shehena lolote litakaloingia nchini humo litakamatwa.
Wasafiri wanaotembelea nchi ya Ujerumani wameonywa dhidi ya kula matango mabichi, kachumbari, nyanya au mboga ambayo haijapikwa. Na kila mmoja ameombwa kwenda hospitali endapo atajihisi kuumwa na tumbo au kuwa na dalili kama hizo.
Profesa Hugh Pennington, mtaalamu wa mikrobiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Aberdeen, anasema kuwa kinachoshangaza ni kwamba maradhi haya hayajawadhuru watoto wadogo.
"kwa kawaida maradhi ya aina hii huwasumbua watoto wenye umri ulio chini ya miaka mitano, lakini kwa sasa wanaelekea kuponyoka.
Afrika
Hakuna habari yoyote kuhusu kama kuna mtu yeyote wala mazao yaliyoathiriwa na bakteria huyu hatari barani Afrika.

No comments:

Post a Comment