Friday, June 3, 2011

Mkulima auawa kinyama Tanzania


Polisi nchini Tanzania inapeleleza mauaji ya meneja na muwekezaji nchini humo Sifael Jackson.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara kaskazini, Parmena Sumari ameiambia BBC kuwa maofisa wake wanaendelea kuwasaka wauaji wa mfanyabiashara huyo.

Mwandishi wa habari Benny Mwaipaja ameiambia BBC kuwa marehemu alivamiwa na kuuawa na genge lililokuwa na mikuki, magongo na mapanga akiwa ndani ya gari lake.
Mauaji haya yanatokea wakati kukiwa na upinzani mkubwa wa raia dhidi ya
mpango wa serikali wa kupigia debe uwekezaji wa kilimo kwa kiwango kikubwa.
Uvamizi

Mwandishi huyo aliendelea kusema kuwa "Bw Jackson aliuawa kinyama na kukatwa kichwa na genge la hadi watu 15 siku ya Jumanne jioni.
Baadhi ya wakaazi wa mkoa huo wa Manyara wanaishutumu serikali kwa kutishia hali yao ya maisha kwa kugawa ardhi yao vipande vikubwa kwa wakulima wa kibiashara wa mashamba makubwa, wakiwemo wakulima wa kigeni.
raia wapinga ardhi kupewa wageni
serikali yataka ardhi itumiwe
Lakini serikali inasema kuwa lengo la sera hiyo ni kujaribu kuimarisha uzalishaji wa chakula na kuhakikisha kwamba ardhi inatumiwa kikamilifu.
Kwa uchache mashamba manne yamevamiwa mwaka huu karibu na mji wa Babati huko Manyara, ambako mazao yalichomwa na mali kuteketezwa kwa moto.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alituma ujumbe mkubwa wa Mawaziri wa serikali kwenda kupeleleza kuhusu mzozo huo.
Ujumbe huo uliwaonya wananchi katika maeneo walioyazuru dhidi ya vitendo vyao vya kuvamia na kuteketeza mali za watu la sivyo watakamatwa na kuhukumiwa.
Mwandishi huyu Mwaipaja alisema kuwa serikali ina wasiwasi kuwa ghasia hizo sasa zinaweza kuikosesha Tanzania wawekezaji ambao ina imani wangeweza kusaidia mpango wake wa kijani.
Kampeni ya serikali ya kutaka kilimo cha kiwango kikubwa kibiashara ni mabadiliko makubwa ukizingatia sera zilizokuwepo baada ya Uhuru zilizokuza na kupendelea Usoshalisti

No comments:

Post a Comment