Monday, June 6, 2011

Ndege yaanguka ikipeleka wagonjwa Samunge, Sunday, 05 June 2011 21:26, waliofariki samunge wafikia 103, maelfu ya watu kutoka Afrika ya Mashariki, Asia na Ulaya wazidi kumiminika kwa BABU.


Mussa Juma, Arusha
NDEGE ndogo ya abiria, iliyokuwa imebeba wagonjwa kuwapeleka Samunge kwa Mchungaji mstaafu Ambilike Mwasapila, imeanguka na wagonjwa kuwajeruhiwa.
Tukio hilo lilitokea juzi mchana, baada ya ndege hiyo ambayo hufanya safari za Arusha- Loliondo, kupoteza mwelekeo na kuanguka Kijiji cha Mgongo Mageri, Kitongoji cha Melau.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Pwapwa, alithibitisha taarifa za ajali hiyo na kwamba, ndege hiyo namba C150 imesajiliwa kwa namba 54MW0.
Mpwapwa alisema taarifa ambazo zilifika polisi, ndege hiyo ilikuwa na watu wawili ambao ni Emmanuel Swai (74), ambaye amevunjika mkono na rubani wa ndege hiyo, Clinton Swai (25), aliyeumia kichwa.
Alisema wagonjwa hao baada ya ajali hiyo, walikimbizwa Hospitali ya Selian mjini Arusha kupata matibabu.

Waliofariki Samunge wafikia 103
Watu wengine wawili, wamefariki dunia juzi Samunge, huku wakifanya idadi ya
watu waliofariki kufikia 103 kuanzi Machi 11 hadi June 4, mwaka huu.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Samunge, Elias Lubida, aliwataja waliofariki kuwa, ni Sultani Seleman (55), mkazi wa Mombasa, Kenya na Celina Shija (4), mkazi wa Kasulu, Kigoma.
“Watu hawa walifariki baada ya kufika Samunge wakiwa mahututi, hivyo kufariki kabla ya kupata tiba,” alisema Lubida.

Wanyarwanda, Wakenya waendelea kutua Samunge
Mamia ya watu, kutoka nchi za Afrika ya Mashariki na nchi nyingine za Ulaya na bara la Asia , wameendelea kutua Samunge kupata tiba.

Watu hao, wamekuwa wakifika kwa usafiri wa magari, ndege na helkopta za kukodi kutoka Arusha.
Hata hivyo, foleni ya magari ambayo yanafika Samunge imeendelea kupungua hasa nyakati za mchana.

No comments:

Post a Comment